Wanawake walioolewa kwa mara ya kwanza ruksa kumiliki ardhi

Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi amebainisha kuwa,wanawake walioolewa kwa mara ya kwanza wanaweza kumiliki ardhi pamoja na waume zao.

Hadi sasa, sera ya ardhi ya nchi hiyo inawazuwia wanawake kumiliki ardhi, kama waume zao tayari wanamiliki ardhi nchini Botswana.

Sheria za nchi hizo zinaeeza kuwa, wanawake ambao bado hawajaolewa ambao hawana ardhi ndio wanaokubaliwa kisheria kumiliki ardhi.

Ubaguzi huo uliwaacha mamilioni ya wanawake bila uwezo wa kupata ardhi katika maeneo wanayoishi na kufanyakazi.

“Kila Mbotswana atakuwa na uwezo wa kupata ardhi ya makazi katika eneo analochagua katika nchi, katika ardhi ya taifa na ya kikabila," ameeleza Rais Masisi kupitia ukuta wake wa Twitter.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news