Kwa sasa, kuna zaidi ya visa milioni 29 vya maambukizi ya virusi vya Corona duniani (COVID-19) na zaidi ya vifo 900,000 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) vimerekodiwa.
Aidha, wakati chanjo ikitajwa kuwa inaweza kuwa ndio mwisho wa janga hilo endapo tu itatengenezwa kwa wingi na kwa ufanisi ili kusambazwa duniani kote, bado wengi wanaendelea kuumiza vichwa.
Pia kuna maswali mengine ya kuzingatia kama itahitajika dozi moja au zaidi ya dozi moja na kwa kiwango gani na kwa muda gani, majibu ya haya maswali bado hayajaweza kupatikana mpaka pale chanjo itakapopatikana, lakini jamii za Kikristo hazijakaa kimya na kukunja mikono kusubiri chanjo.
Septemba 16,2020 waumini wa Kanisa la Shincheonji Chuch of Jesus, kanisa lenye maelfu ya waumini kutoka nchi mbalimbali duniani waliandaa ibada ili kusali kwa ajili ya kumuomba Mungu kuiondoa kabisa Corona na kuwezesha upatikanaji wa tiba yake.
Pia kuwaombea waanga wa virusi hivyo vya COVID-19 na familia zao, wauguzi pamoja na maafisa wa Serikali.
Ibada hiyo kwa njia ya mtandaoni ilirushwa mubashara kwa waumini wote zaidi ya milioni mbili duniani kote ambapo walijumuika pamoja ikiwemo Marekani, Uingereza, Korea Kusini, Australia, Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe.
Kwa kufuata utaratibu uliowekwa na maafisa wa afya kama kukaa mita zaidi ya mbili, utaratibu huo ulifuatwa ili kuwalinda waumini dhidi ya virusi hivyo, Shincheonji iliandaa hilo kusanyiko kwa njia ya mtandao na waumini wao kuweza kusali pamoja kwa usalama na kuwa kama mfano kwa wengine.
Maombi yalikuwa zaidi kwa uponyaji kwa wale walioambukizwa virusi hivyo,maafisa na wafanyakazi wa afya ambao wanafanya kazi kwa kupitiliza kupambana dhidi ya Corona na kwa wale wenye msongo wa mawazo kiuchumi kutokana na janga hilo, wingi wa kusanyiko hilo mtandaoni kwa waumini wa Dunia nzima umeonyesha uhitaji wa haraka wa kumaliza virusi hivyo na kuponya na kurudisha jamii kama awali.
Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji Church of Jesus, Lee Man hee aliyependekeza kusanyiko hilo mtandaoni amesema, waumini wote waendelee kusali katika misa za kuabudu hadi virusi hivyo vitakapoondolewa.
Mwenyekiti wa Kanisa la Church of Jesus, Lee Man hee |
Hata hivyo, zaidi ya waumini wa 1700 wa kanisa hilo ambalo makao makuu yake yapo Korea Kusini wamejitolea utengili (blood plasma) kwa ajili ya utafiti wa matibabu ya virusi hivyo.
Utengili umeleta matumaini kama tiba dhidi ya corona kwani inaaminika imepunguza dalili hatarishi za wagonjwa walio kwenye hali mbaya.
“Ili kushinda ugonjwa wa Corona tunahitaji upendo na umoja,kwa umoja wetu tulitaka kufanya yote tunayoweza kama waumini, kubwa zaidi ni kwa kusali kwa ajili ya watu wanaofanya kazi kudhibiti maambukizi ya gonjwa hili na wafanyakazi wa afya wote wanaofanya kazi na waliopo mstari wa mbele kwenye hii vita dhidi ya Corona na tunaamini Mungu atajibu maombi yetu,”amesema.
Sala hizo zimekuwa ni jambo la kawaida ndani ya kanisa hilo la Shincheonji wakati taasisi za afya zikiwa zinaendelea na mapambano ya kupatikana kwa chanjo na tiba inayohitajika ili kutokomeza virusi hivyo vya corona duniani.