Waziri wa Madini,Doto Biteko amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) katika Mkoa wa Geita umesaidia kuleta ufanisi katika shughuli za uchimbaji madini,anaripoti Robert Kalokola,Geita.
Biteko
amelipongeza shirika hilo kwa kufikisha umeme kwenye maeneo ya uchimbaji dhahabu katika Mkoa wa Geita hususani maeneo ya wachimbaji
wadogo .
Waziri Biteko
ameyasema hayo leo alipotembelea banda la TANESCO katika Maonesho ya
Teknolojia ya Uchimbaji Madini yanayoendelea katika Kijiji Maalum cha
maonyesho katika mji wa Geita mkoani hapo.
"Nishati ya umeme imekuwa chachu ya kuongeza ufanisi katika uchimbaji madini,"amesema Waziri Biteko.
Septemba
18, mwaka huu TANESCO iliwasha kituo chake kikubwa (Substation) cha
kupozea na kusambaza umeme cha Mpomvu Mjini Geita kinachopokea umeme wa
Kilovoti 220 kutoka Bulyanhulu.
Moja ya transfoma inayotumika kupoza umeme katika Kituo cha Mpomvu mjini Geita.(Diramakini). |
Umeme
unaotoka katika kituo hicho unasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita ambao kwa mujibu wa TANESCO umemaliza tatizo la uhaba wa
umeme katika mkoa huo.
Moja ya maeneo yanayonufaika na umeme huo ni kwenye migodi ya wachimbaji wadogo ndani ya Mkoa wa Geita.
Katika
ziara hiyo, Waziri Biteko aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert, viongozi na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya
Madini.
Maonyesho ya Teknolojia ya Uchimbaji Madini yalianza Septemba 17, mwaka huu na yatahitimishwa Septemba 27, mwaka huu.