Mgombea Urais kupitia Chama cha ADC ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa na Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashi akiwa katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na tume kuwania nafasi ya urais. Mheshimiwa Rashid alifika ofisi za tume leo Septemba 9, 2020. Mgombea huyo amekaririwa na www.diramakini.co.tz akirejea msimamo wa chama chake kuwa, iwapo wananchi watakipa chama hicho ridhaa, watayafurahia matunda ya uongozi bora, kwani "Katika kuelekea uchaguzi Mkuu 2020, ADC sera zetu sisi ni za Digital Economy. Kila siku tunasema sisi ADC asilimia 70 ni vitendo na asilimia 30 pekee ndio maneno. Hiki ndio chama chetu, hatuna longo longo sisi."Nirejee kutoa wetu kwa wananchi, viongozi wenzangu pamoja na vyombo vya dola kwa pamoja tusimamie amani ya nchi yetu na tusikubali kuivuruga,"anasema mgombea urais wa Zanzibar kupitia ADC, Hamad Rashid.