Waziri Kigwangalla, Balozi wa Marekani wajadili kuhusu utalii Tanzania



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright kuelezea mafanikio ya Tanzania katika Uhifadhi wa Maliasili na utayari wa Tanzania kupokea Watalii kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani wakati huu wa janga la Corona. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright (kushoto) na ujumbe wake kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa kulinda maeneo yaliyohifadhiwa,kudhibiti ujangili pamoja na Taifa kuendelea kunufaika kimapato, kutoa fursa za ajira na uwekezaji kwa Watanzania na Wageni akimwomba Balozi huyo asaidie kuhamasisha raia wa Marekani waje kuwekeza nchini Tanzania.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt.Donald Wright (kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) walipokutana kwa mazungumzo mafupi yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano na uendelezaji wa shughuli za uhifadhi baina ya Tanzania na Marekani leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Aron Msigwa-WMU.




Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news