WAZIRI UMMY MWALIMU: SITAWAJIBU, ACHA WANITUKANE, LAKINI NINAENDA KUWA CHACHU YA MAENDELEO

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu (CCM) amesema kwamba kamwe hatawajibu wanaomtukana kwenye majukwaa badala yake ataeleza namna nitakavyoweza kuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wakati akipewa ridhaa ya kuwaongoza, anaripoti MWANDISHI WETU.

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo leo wakati semina hiyo itasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi semina hiyo imeandaliwa na Shirika la Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) ikiratibiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye pia ni mgombea ubunge Jimbo la Tanga kupitia CCM akizungumza wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa wagombea wanawake kwa nafasi za ubunge na udiwani , ambayo itasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi semina hiyo imeandaliwa na Shirika la Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) ikiratibiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation, Neema Lugangira (kushoto) na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Rehema Maro.

Amesema kwamba, atakachokifanya wakati akiendesha kampeni zake za kuwania ubunge jimbo hilo atajikita kwenye kueleza namna atakavyosaidia wananchi kuweza kujikwamua kimaendeleo kwa kuona namna ya kushirikiana nao katika kufikia mafanikio.

“Niseme tu kwamba nitakapokuwa kwenye kampeni sitatumia jukwaa kuwajibu ambao wananitukana badala yake nitajikita kwenye kutangaza maendeleo makubwa na mipango ambayo nitawafanyia wananchi wa Jimbo la Tanga, lakini pia niwashukuru wajumbe wa UWT kwa sapoti kubwa kwangu,”amesema.

Sehemu ya washiriki wa semina hiyo,

Amewaomba wanawake wanaowania uongozi kwenye nafasi mbalimbali wasiwe mawakala wa kuwatukana watu ikiwemo kuwadhalilisha wanawake wenzao na "ukisikia neno limesemwa mwananke unakuwa wa kwanza kulishikia bango, hiyo sio sawa hakikisheni mnabadilika".

Waziri Ummy amewataka pia kuhakikisha hawawi mawakala wa kusambaza mambo ya ovyo yanayodhalilisha utu na haki ya wanawake kwa sababu wao ndio walezi wa familia na ndio watapambanaji ambao wanalea familia, hivyo watambue wana umuhimu mkubwa kwenye jamii

“Ndugu zangu tusifanye kampeni za matusi za kudhalilisha wanawake wenzetu kwenye majukwa, lakini niwaambie kwamba wakati wa kampeni zangu hawatanisikia nikiwajibu ambao wananitukana badala yake nitajikita kwenye kutangaza namna nitakavyoleta maendeleo,”amesema Ummy Mwalimu.  

Pia amewataka wanawake kuhakikisha wanasaidiana, kuacha kuoneana wivu na choyo badala yake washirikiane katika kujiletea maendeleo ambayo yatawasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii ambazo zinawazunguka.

Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga,Sophia Nkupe akizungumza wakati wa semina hiyo.

Ummy aliwaomba wakati mwengine kuipeleka semina hiyo katika mikoa mingine wanawake kuwa mstari wa mbele kupigania vipaumbele vya wanawake katika afya ya mama na mtoto, elimu kwa watoto wa kike kwa lengo la kuweza kuwakomboa

Awali akizungumza wakati wa semina hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation, Neema Lugangira amesema, wamejikita kutoa elimu kwenye masuala ya lishe na kuhamamisha kilimo lishe.
Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation, Neema Lugangira akizungumza wakati wa semina hiyo.

Amesema kwamba, mwaka juzi walianza mchakato maalumu wa kisera kuhakikisha ajenda hiyo inaingia kikamilifu kwenye ilani ya uchaguzi na kwa mafanikio ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 ajenda ya lishe imeingia kikamilifu kwani imekuwa kati ya vipaumbele vikubwa ya CCM.

Lugangira amesema,watoto wanapokuwa na lishe duni hiyo ni changamoto, kwani ndio nguvu kazi ya kesho ili Taifa lolote listawu lazima kuwepo na nguvu kazi thabiti ya kiuchumi.

Amesema, ajenda ya lishe imepata nafasi yake maalumu kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kati ya malengo ni kushuha hali ya udumuvu hadi kufikia kiwango cha asilimia 24 ndani ya miaka mitano ijayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news