SHULE za msingi za Biyungu na Kilruruma wilayani Karagwe mkoani Kagera ni miongoni mwa shule zilizokuwa na changamoto kubwa ya vyoo vya wanafunzi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wananfunzi licha ya Shirika la World Vision Tanzania kusaidia katika sekta hiyo, anaripoti ALLAWI KABOYO-KAGERA.
Katika hafla ya kukabidhi matundu manane ya vyoo kwa kila shule yaliyojengwa na shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania, Mradi wa Bushangaro AP kwa serikali ya mkoa,meneja wa shirika hilo Kanda ya Kagera, Juliana Charles amesema kuwa, walifika katika shule hizo na kusikitishwa na hali waliyoikuta na kuwiwa kuanzisha ujenzi wa vyoo hivyo.
Juliana amesema kuwa, shirika hilo linajihusisha zaidi na makuzi ya mtoto hivyo kujenga miundombinu ya vyoo shuleni ni moja ya huduma muhimu kwa mtoto ambayo itampelekea kusoma kwa raha, lakini pia kuweza kumuepusha na magonjwa mbalimbali ya mlipuko yanayoweza kumtokea.
Sambamba na ujenzi wa vyoo hivyo, shirika hilo pia limekabidhi mradi wa maji ambayo mtandao wake umesambazwa kwenye vijiji viwili ambavyo vipo Kata ya Bushangaro na kuweza kusambazwa katika zahanati ya Nyakagoyagoye ili kuweza kurahisisha huduma hiyo kwa jamii ya Wanakaragwe. World Vision Tanzania imekuwa mwanga wa maendeleo soma hapa.
Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Profesa Faustine Kamzora baada ya kukabidhiwa miradi hiyo ameitaka jamii kuitunza miradi na kutunza mazingira ili kuhakikisha ubora wa miradi unabaki ulele ule ambapo pia ameutaka uongozi utakaosiamamia mradi wa maji kuhakikisha maji hayo wanayatibu kabla ya kumfikia mwananchi ili kumuepusha na magonjwa.
Profesa Kamzora amesema, mradi umejingwa kwa ufadhili wa nchi ya Ujerumani kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 400 na endapo mazingira ya miundomibun ya maji yakiwekwa kwenye hali ya usafi unaozingatia matunzo bora unaweza kuondoa magonjwa yanatokana na matumbo hasa kwa watoto wadogo.
Amesema,vituo vya afya na hospitali na zahanati kwa asilimia kubwa zinapokea matatizo ya magonjwa ya upungufu wa maji kwa asilimia 70 pamoja nna magonjwa ya tumbo kutokana na watu kutumia maji ambayo sio salama ambayo yote hayo ni ukosefu na uhaba wa maji yenye uhakika.
Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Kagera, Juliana Charles amesema, mradi huo utahudumia wananchi ambao awali walikuwa wakitumia muda mrefu kufuata maji vijiji jirani ambayo bado yalikuwa hayapo katika usalama.
Charles amesema kuwa,”baada ya kupatiwa taarifa na kamati ya maji kijijini hapo, shirika liliweza kufika eneo la chanzo na kufanya tathimini ya shughuli ya ujenzi utakaoweza kuzua mifugo isiweze kuingia ndani ya maji hayo kwa kuyazumguzisha.
Shirika limefanya ujenzi wa chanzo kwa kujengea maji ikiwa ni kuzuia mifugo,na kutunza chanzo kisiweze kuharibiwa na jamii ambayo inatakiwa yenywe itunze chazo hiki”.
Mwenyekiti wa Kjiji cha Nyakagoyagoye, Salmoni Mtilani amesema, kukamilika kwa ujenzi huo utaondoa watoto kutumia muda mwingi kutafuta maji na wakati mwingine kutokuhudhuria shuleni kwa ajili sababu ya wazazi wao kuwatuma maji umbali mrefu.
“ Sio watoto sio wazazi wao wanatembea umbali mrefu wa kilomita18 kwenda kijiji jirani kufuata maji ambayo hayachangamani na mifugo., kijingine ni watoto kutohudhulia shuleni kabisa na kuwafanya kukosa masomo na hatimaye kushuka kitaaluma,”amesisitiza Mtilani.
Mtilani amesema kuwa, Kijiji cha Nyakagoyagoye kilikuwa kinafuata maji kijiji jirani kwa sababu chanzo ambacho kimefanyiwa ujenzi wanajamii walikuwa wanayatumia kama maji ya mifugo kwa mazinmgira yalikuwa hayaridhishi kwa wanajamii kwenda kuchota maji hayo.