KLABU ya Yanga SC leo Septemba 11, 2020 imezindua jezi mpya kwa ajili ya msimu wa
2020/21, uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Fredrick Mwakalebela ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC amesema kuwa,wale ambao watachakachua jezi hizo watachukuliwa hatua mara moja.
Amesema, msimu huu wameandaa kikosi kazi ambacho kinafanya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuhakikisha hakuna ambaye anafanya hujuma katika jezi zao.
”Tumekuwa timu ya kwanza kuzindua duka la vifaa vya Yanga SC pamoja na jezi nzuri na yenye ubora, hivyo tupo imara katika kila idara na tunaamini kwamba tutafanya mengi makubwa,"amesema.
Tags
Michezo