Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo , Zitto Kabwe amesema vyama vya upinzani nchini vimekubaliana kumuunga mkono Mgombea mmoja wa Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na pia, kwa upande wa Zanzibar.
Zitto ameongeza kuwa Oktoba 3, 2020 watatangaza ni nani hasa atasimama kama Mgombea Urais katika mkutano wa hadhara utakaohusisa CHADEMA, ACT Wazalendo na vyama vingine vya upinzani.
Amesema ACT-Wazalendo wameshajadiliana na wameshawasilisha mapendekezo yao kwa CHADEMA na baada ya pande zote kukamilisha mazungumzo watatangaza makubaliano yatakayofikiwa.