Ni wazi kuwa kila mmoja wetu anatamani kuwa na familia bora ambayo itaongeza furaha katika familia na pengine katika ndoa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kila mmoja ukikaa naye japo dakika moja, iwe jinsia ya kiume au ya kike ukamuhoji juu ya tamanio la maisha yake ya baadae, jibu la haraka litakuwa ni kumuomba Mungu kuwa na familia bora, hii ni sawa kabisa.
Hiyo ndiyo ndoto ya kila mwanadamu, maana hata vitabu vitakatifu vimeelekeza kuwa, enendeni Ulimwenguni mkazaliane na kuongezeka, hii kuongezeka huwa haitokei ghafla tu, bali ni hatua inayojumuisha jinsia mbili tofauti yaani mke na mume ambao wametimiza taratibu zote za kijamii, kiimani na kifamilia kuunganishwa kuwa mwili mmoja.
Baada ya kuunganishwa huko, wengi wetu tumekuwa tukishuhudia namna ambavyo, mategemeo ya familia nyingi yakiwa kwa wawili hao, kubwa likiwa ni kuhusu watoto, inapotokea wanandoa kukawia kukosa watoto, macho ya wanajamii huwa yanaelekezwa kwao, bila kujua sababu au chanzo cha kuchelewa huko, wengine huwa wanaanza lawama, lakini tafiti nyingi zimebainisha kuwa, kwa namna moja au nyingine upungufu wa nguvu za kuliwezesha tendo lile lenye matokeo ya kupata baraka ya watoto linachangiwa sana na mifumo ya maisha yetu.
Pengine sababu kubwa pia ni pamoja na aina ya vyakula tunavyotumia au aina fulani ya maisha tunayoishi kila siku, ili kuwasaidia wale ambao wanakabiliwa na changamoto hii kuu na hata wale ambao wameathirika kwa kujichua, Diramakini inakusogezea aina ya matunda au vyakula ambavyo vina uwezo wa kukupa nguvu ili uweze kurejea katika hali ya kawaida na matokeo yakaonekana katika familia.
Mosi ni tunda la parachichi, ili ni tunda ambalo watafiti wamebaini kwamba lina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume na kuimarisha tendo la ndoa.
Watafiti wa mambo wanabainisha kuwa,ndani ya parachichi kuna utajiri mkubwa wa vitamini E, hii ni vitamini ambayo huwa inasaidia katika uzalishaji wa homoni zinazosaidia kuongeza nguvu za kiume.
Watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali hasa wakati wa kushiriki tendo la ndoa, hivyo linapendekezwa kutumika kwa wanaume na wanawake, mwishowe watapata matokeo mazuri. Pia kwa wanawake, husaidia kuongeza majimaji yaliyo na utelezi katika sehemu za siri za mwanamke ili kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa tendo la ndoa, hivyo kumfanya naye kulifurahia tendo hilo.
Pili ni matumizi ya karanga, wakati wengi wetu tumekuwa tukiziona karanga kama jambo la kawaida, tafiti zinabainisha kuwa, zina utajiri mkubwa wa protini mwilini.
Kwa mujibu wa wataalamu, karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia mwili kuwa na mfumo wa damu unaohitajika.Hatua ambayo huwa inawezesha matokeo mazuri katika hatua za ushiriki wa tendo la ndoa, hivyo unashauriwa kuzitumia karanga kwa wingi, wala usipuuzie kwa matokeo mazuri.
Jambo la tatu ni matumizi sahihi ya kitungu swaumu, hiki kitunguu huwa kina sifa kuuwa zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini, kutokana viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.
Miongoni mwa viasili hivyo husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu,husaidia kudhibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.
Pia kitunguu swaumu kina allicin, kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzunguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi, wataalam wanasema,kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu, hatua ambayo uwezesha kupata matokeo mazuri.
Hatua ya nne ni matumizi ya pweza au ngisi ambao ni aina za samaki ambazo huvuliwa baharini, samaki hawa huwa na madini ya zinc na chumvi kwa wingi, madini hayo yanajulikana kwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinanvyoleta msisimko wa mwili wakati mume na mke wanashiriki tendo la ndoa.
Tano ni ndizi, unapofikiria kufyanya vyema katika tendo la ndoa, unatakiwa kuwaza kuhusu uimara wa misuli ya mwili ambayo hutajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye umuhimu mkubwa katika kushiriki tendo la ndoa.
Tambua kwa hatua hiyo, hulaji wa ndizi mbivu husaidia kujenga misuli ya mwilini na pia kumfanya manamume kuwa hodari katika tendo la ndoa, hivyo unashauriwa kupata kwa wingi.
Jambo la sita ni matumizi ya Chocolate, huwa na viamabato kama vile alkaloid na phenylethylamine, aina hii ya viambato huongeza stamina ya kushiriki tendo la ndoa, Phenylethylamine husaidia mtu kuhisi vizuri wakati wa kushiriki tendo hilo.Kwa hiyo, kama una tatizo la kutoshiriki tendo la ndoa vizuri, jaribu kula chocolate mara kwa mara utapata matokeo bora.
Aina ya saba ni ulaji wa tikiti maji, hili ni tunda ambalo lina faida nyingi sana kati mwili wa mwanadamu, mosi tunda hili ni huwa na virutubisho kama vile potasium, calcium, magnesium, carotene, zikiwemo vitamini muhimu kama vitamini A, B6, na C. Hivyo, tikiti maji hususani mbegu zake wataalam wanasema usaidia kuupa mwili chembechembe muhimu za kuongeza nguvu za kiume mwilini. Ndiyo maana unashauriwa kuyatumia mara kwa mara kwa faida zaidi.
Aina ya nane ni mbegu za matunda, huu ni mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za matunda kama ile maboga, tikiti maji au mengine ambayo husaidia kupunguza asidi mwilini na kumfanya mtu awe na afya njema.
Jambo la tisa ni mvinyo mwekundu, utafiti umedhihirisha kuwa mvinyo mwekundu una wezo wa kuongeza msukumo wa damu,tambua kuwa kiwango cha msukumo wa damu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa uume umesimama wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Aidha,jambo la mwisho ni matumizi ya tangawizi ambayo husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, tangawizi inatajwa kuwa na faida nyingi mno katika kufanikisha tendo la ndoa kuwa na matokeo mazuri.