AirUganda na ujio wa Airbus A330-800, hongereni viongozi kwa maono chanya

Pongezi za dhati kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa kuendelea kuiheshimisha nchi yake, ukimya wa Shirika la Ndege Uganda ulikuwa na mfanano wa miaka mingi na Shirika la Ndege Tanzania ambalo kwa sasa chini ya Rais Dkt.John Magufuli, Watanzania na Dunia inafahamu kilichojiri,sasa AirTanzania ni miongoni mwa mashirika ya ndege yanayokuja kwa kasi kubwa zaidi barani Afrika na pengine Duniani, anaripoti Mwandishi Diramakini.
"Ujio wa ndege mpya ya Airbus A330-800 kwa Shirika la Ndege Uganda si jambo dogo, ni jambo kubwa ambalo linafaa sana kupongezwa,wengi wetu wanaweza kubeza hatua hii, lakini ubezaji huo hauondoi ukweli kwamba, shirika linakwenda kupiga hatua. Nichukue nafasi hii kumpongeza sana Rais wetu Mheshimiwa Museveni kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji huu wenye mafanikio makubwa kwa ajili ya Taifa na umma wote ndani na nje ya Uganda. 
"Mafanikio haya ninaamini yanakuja kutokana na ile mbegu ya uzalendo iliyopandikizwa kwa baadhi ya viongozi wetu na Rais mpendwa sana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, aliyeonyesha njia ya kweli katika uwekezaji katika usafiri wa anga, mwishowe tumeona matamanio ya kila mmoja akijifunza juu ya hayo na kutenda, kwani baada ya kuliwezesha shirika la umma la ndege Air Tanzania kupiga hatua ndani ya Afrika Mashariki, mwelekeo ndio huo huo kwa viongozi wengine, niwapongeze sana viongozi wetu hawa kwa maono mapya na matamanio mapya kwa ajili ya mataifa yetu, kwani sisi Wana Afrika Mashariki ni ndugu wamoja, kila linalofanyika lenye heri tunasherehekea pamoja,"anafafanua Mussa ambaye ni raia wa Uganda anayeishi nchini Tanzania katika mahojiano mafupi na Mwandishi Diramakini.
Hata hivyo, juhudi za Mwandishi Diramakini kukuletea taarifa zaidi zinazojiri wakati ndege hiyo kubwa ikisubiriwa kuwasili jijini Kampala wakati wowote zinaendelea, endelea kufuatilia hapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news