Zaidi ya watu 20 wanaripotiwa kufariki dunia baada ya basi kugongana na treni Oktoba 11,2020 nchini Thailand, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wananchi,vikosi vya usalama wakiangalia namna ya kutoa msaada katika eneo la ajali hiyo. (AFP).
Mamlaka nchini humo zimethibitisha kuwa, basi hilo lilikuwa linakatiza katikati ya reli iliyopo zaidi ya kilomita 63 Mashariki mwa mji mkuu wa Thai, Bangkok. Ripoti za awali zimebainisha kuwa, treni hiyo ilikuwa imebeba wafanyakazi 60 ambapo tayari watu 30 waliojeruhiwa vibaya wanaendelea na matibabu.
Gavana wa Jimbo la Chachoengsao, Maitree Tritilanon amesema, eneo hilo ambalo ajali imetokea, mamlaka zitaangalia namna ya kufanya ili kuhakikisha kuwa, ajali kama hiyo haijirudii tena ikiwemo kuweka alama za kuonyesha hatari kabla na baada ya kuvuka
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Taifa la Thailand linatajwa kuwa na visa vingi vya ajali za barabarani duniani.