Baada ya kupitia katika kipindi kigumu kifedha, hatimaye
Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) ya mkoani Kilimanjaro imeingia
mkataba wa makubaliano na Benki ya CRDB ya uwekezaji huku kiasi cha shilingi bilioni saba kikiwekezwa katika benki hiyo, anaripoti Dixon Busagaga
,Kilimanjaro.
Hafla ya makubaliano hayo imefanyika mjini Moshi na
kuhudhuriwa na watendaji wa benki hizo mbili wakiwemo wenyeviti wa bodi
za Wakurugenzi ,Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Bernad Kibese,mgeni
rasmi katika hafla hiyo iliyoenda sambamba na zoezi la ukataji wa utepe
katika Benki ya KCBL akiwa ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashatu Kijaji.
Katika hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela iliyosomwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa
Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo amesema, Benki ya CRDB imekua mstari
wa mbele katika kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo katika
utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kimaendeleo iliyolenga kukuza
uchumi wa Mtanzania na nchi kwa ujumla wake.
Mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na KCBL ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt.Ashatu Kijaji akikata utepe katika jengo la Benki ya KCBL kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za kibenki mara baada ya makubaliano baina ya benki hizo mbili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL), Dkt.Gervas Machimu (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya CRDB, Dkt.Ally Laay wakifanya makabidhiano ya nyaraka za makubaliano baina ya benki hizo mbili.
Mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na KCBL ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt.Ashatu Kijaji akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mjini Moshi.
Baadhi ya wanachama wa vyama vya Ushirika na AMCOS na SACCOS waliofika kushuhudia hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) iliyofanyika mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt.Anna Mgwira akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) iliyofanyika mjini Moshi.
Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt.Bernad Kibese akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) iliyofanyika mjini Moshi.
Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini, Dkt.Benson Ndiege akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) iliyofanyika mjini Moshi.
Baadhi ya wanachama wa vyama vya Ushirika na AMCOS na SACCOS waliofika kushuhudia hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) iliyofanyika mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) iliyofanyika mjini Moshi.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB,Fredrick Nshekanabo akiwasilisha hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) iliyofanyika mjini Moshi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Ashatu Kijaji (katikati wailiokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Benki ya CRDB ,Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCBL Dkt ,Gervas Machimu ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB ,Dkt Ally Laay,Naibu Gavana wa Benki kuu ,Dkt Bernad Kibese na Miwsho ni Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege.
Mgeni rasmi katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB na Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt, Ashatu Kijaji (katikati wailiokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) ,Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCBL Dkt ,Gervas Machimu ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB ,Dkt.Ally Laay,Naibu Gavana wa Benki kuu ,Dkt Bernad Kibese na Miwsho ni Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege.
“Ushiriki wetuu na
utiaji saini mkataba wa uwekezaji kati ya CRDB na Benki ya ushirika ya
KCBL ni udhihirisho wa wazi wa adhma ya benki kukwmua jamii kiuchumi na
kujenga sekta tumanini na tabasamu kwa wadau ,wateja na wana hisa wa
benki ya KCBL.” amesema Nsekela.
“Huu utakuwa mwanzo mpya kwa
KCBL kwa Taifa na Serikali ya awamu ya tano ,leo njozi ya muda mrefu ya
kuwa na benki ya ushirika nchini umetimia.”ameongeza Nsekela. Amesema, benki ya CRDB kama raia mwema mwenye dhamira njema kwa nchi
yake itatumia sehemu ya mtaji wake kuwekeza KCBL bila kuchukua faida
wala gawio kwa kipindi cha miaka 3 ili kuikwamua ki mtaji ,kuongeza
ukwasi na kuismamia menejimenti,na utawala bora.
“Uwekezaji huu
unalenga kuhakikisha benki inajiendesha kwa ufanisi na faida ili kuvutia
uwekezaji mpana wa kimtaji toka wana ushirika na vyama vya akiba na
mikopo ,Msaada wa benki ya CRDB pia utahusisha kuboresha rasilimali watu
na uendelevu wa menejimenti pale mda wa uwekezaji utakapokoma,"amesema
Nsekela.
“Ni wazi kuwa uimara wa uchumi wa nchi unategemea kwa
kiasi kikubwa uimara wa taasisi za fedha na hivyo kama Benki kiongozi
nchini tunao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa tunashirikiana kwa karibu
na serikali katika kuhakikisha sekta ya fedha inabaki kuwa imara na
salama wakati wote,”amengeza Nsekela.
Nsekela amesema pamoja na
CRDB kwenda kufanya uwekezaji wa kimkakati katika benki ya KCBL ,bado
CRDB inaona kilichofanyika ni zaidi ya uwekezaji kwa kusimama katika
nafasi kama benki kiongozi na kutekeleza jukumu la kulinda uimara na
usalama wa sekta ya fedha nchini .
“Tunaimarisha ushirika kama
nyenzo muhimu ya maendeleo kwa jamii na kufufua huduma za kifedha kwa
vyama vya akiba na mikopo na katika kipindi cha uwekezaji wake ,Benki ya
CRDB itatumia rasilimali watu na fedha ili kuifanyia maboresho ya
kimkakati ,kimfumo na kimenejimenti benki ya KCBL,"amesema Nsekela.
“Tunaboresha dhima na dira yake kutoka kwa benki ya ushirika katika
mkoa wa Kilimanjaro na kuwa benki ya ushirika Tanzania kwa ajili ya wana
ushirika Tanzania,”almengeza Nsekela.
Mgeni rasmi katika hafla
hiyo ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji amesema Benki
ya CRDB inaelewa nguvu iliyopo kwenye mfumo mzima wa ushirika na kuamua
kwa usahihi kabisa kutumia nyenzo ya ushirika kama mkakati wa
kuwafikishia watanzania wa kawaida huduma za kibenki.
“Sasa hivi
ukitembelea katika vyama vya Ushirika utakuta CRDB Wakala wanafanya
kazi pale ambayo pia ni fursa kwa Ushirika,"amesema Dkt.Kijaji.
“Niwapongeze Wanakilimanjaro hususani vyama vya Ushirika kwa kuunganisha
nguvu na kuanzisha Benki hii ya ushirika (KCBL),pamoja na misukosuko
ambayo benki hii imepitia kwa kisi Fulani ili saidia kuleta nuru kwa
vyama vya ushirika na wanaushirika hasa ukizingatia benki hii ndio
muasisi wa mfumo wa stakabadhi ghalani,"ameongeza Dkt.Kijaji.