Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kawe amemtangaza Askofu Josephat Gwajima kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndiye mshindi wa jimbo hilo kwa kupata kura 194,833 na kumshinda Halima Mdee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura 32,524, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ushindi wa Askofu Gwajima ni sawa na asilimia 84.02 huku Halima Mdee akiambulia asilimia 14.02 ya kura tajwa hapo juu.
Ushindi wa Askofu Gwajima ni sawa na asilimia 84.02 huku Halima Mdee akiambulia asilimia 14.02 ya kura tajwa hapo juu.
Matokeo hayo yametangazwa leo Oktoba 29,2020 na Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Kawe lililopo jijini Dar es Salaam, Aron Kagurumjuli.
Tags
Habari