Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa, limepokea malalamiko ya Klabu ya Yanga SC kuhusu uhalali wa mkataba kati ya Simba SC na mchezaji, Bernard Morrison, anaripoti Mwandishi Diramakini.Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo leo Oktoba 1, 2020.
Ameeleza kwa kifupi kuwa, "malalamiko hayo yanafanyiwa kazi kwa mujibu wa taratibu," Ndimbo amebainisha.
Frederick Mwakalebela ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC amesema hayo leo Oktoba 1,2020 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.
Ameeleza kuwa,wakati klabu yao ikipokonywa haki ya umiliki wa Bernard Morrison wamebaini mapungufu makubwa katika mkataba wa mchezaji huyo na Simba SC.
Fredrick Mwakalebela ambaye amekuja na nakala anayodai ni ya mkataba huo amesema sehemu zote za mkataba huo zimesainiwa na mchezaji huyo pekee hatua ambayo sio sahihi kwa mujibu wa taratibu.
Pia amesema,katika mkataba huo hauna sehemu iliyosainiwa na kiongozi yoyote wa Bodi ya Simba SC, lakini pia hauna saini ya shahidi. Amesema katika kila nakala imesainiwa na Bernadr Morrison pekee bila upande wa pili hatua ambayo inaoonyesha Simba SC hawakuridhia mkataba huo.
"FIFA inamtambua Morrison ni mchezaji wa Yanga. TMS ya FIFA inamtambua Morrison mchezaji wa Yanga. Mkabata wa Simba na Morrison una dosari, upande wa mchezaji umesainiwa bila shahidi,”amesema.
Usajili wa Bernard Morrison kutoka Yanga SC kuibukia Simba SC umekuwa na vituko vingi tangu awali ambapo mwanzo kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya mchezaji na Yanga SC.