Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ambaye ameonyesha kupuuzia wito wa Jeshi la Polisi leo Oktoba 2,2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mgombea huyo amesema kuwa,"wito
wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo
unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa. Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa
na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa
mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi
kesho,"amesema Lissu.
Kauli hiyo ya punde ya Tundu Lissu inakuja kufuatia wito wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro la kumtaka kuripoti leo Polisi.