Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe leo Oktoba 10,2020 ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, ikiwa ni baada ya kupatiwa matibabu kwa siku chache kutokana na ajali mbaya aliyopata akiwa na viongozi wengine wa chama wakielekea katika kampeni, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ilikuwa ni Oktoba 6,mwaka huu ndugu Zitto alipata ajali ya gari akitoka Kata ya Kalya kwenda Lukoma iliyopo Jimbo la Kigoma Kusini.
Aidha, baada ya ajali hiyo ya Oktoba 6, mwaka huu majeruhi wote walipatiwa huduma ya kwanza Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Uvinza baadae Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni na Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
"Nimeruhusiwa kutoka hospitali. Nawashukuru madaktari na wauguzi Kituo cha Afya Kalya - Uvinza, Hospitali ya Maweni Kigoma na Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. Asanteni sana wote kwa Dua, Sala na maombi yenu. Nataraji kurudi kwenye kampeni siku chache zijazo In Sha Allah,"ameeleza ndugu Zitto Zuberi Kabwe.