CCM yawasha mitambo ya Megawatts 1000 Mtwara Mjini,Dkt.John Magufuli, Hassan Mtenga, madiwani watajwa zaidi Oktoba 28,2020



"Tumewasha mitambo ya Megawatt 1000, hii ni mitambo yenye kasi kubwa zaidi, ndiyo maana unaona maelfu kwa maelfu wanasisitiza kuwa Oktoba 28,2020 wanaenda kuunganisha umeme ili kupata kikosi kazi cha kuwahudumia, hii ikiwa na maana kuwa mafiga matatu ndiyo kila kitu, tunatambua mchango mkubwa wa kiongozi wetu Mheshimiwa Dkt.John Magufuli, hivyo tunaamini kwa kushirikiana na vijana wake kina Hassan Mtenga na madiwani wa CCM, Mtwara Mjini mpya inakwenda kustawi katika nyanja zote, hatutafanya makosa tena,"mmoja wa wananchi amemueleza Mwandishi Diramakini.


Wakati huo huo zaidi ya wanachama 1000 wa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mtwara Mjini mkoani Mtwara kwa madai kuwa CCM ndicho chama chenye sera ambazo zinagusa maisha ya kila Mtanzania moja kwa moja.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa mwendelezo wa kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hassan Mtenga ambapo mgombea huyo ameendelea kunadi sera na ilani ya chama hicho huku akiwaomba wananchi waweze kumpa kura, madiwani na mgombea Urais Dkt.John Magufuli.

Akiwa katika mkutano wa hadhara ambao uliwakutanisha maelfu ya wananchi katika Kata ya Tandika,Mtenga mbali na kuwakaribisha wanachama hao alisema, iwapo wananchi watawapa ridhaa, amedhamiria kushirikiana nao kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili. 

"Msikubali kupoteza kura zenu, hakikisheni ikifika Oktoba 28,mwaka huu mapema asubuhi mnapiga kura kwa usahihi, ubunge nipeni mimi kura nyingi, madiwani wapeni wagombea wa CCM kura nyingi na Mheshimiwa Dkt.John Magufuli mpeni kura za kutosha katika nafasi ya Urais.

"CCM ndicho chama pekee ambacho sera na ilani yake inatekelezeka kwa vitendo, ninyi ni mashuhuda namna ambavyo utekelezaji wa Ilani inayoisha ilivyotekelezwa, hivyo tarajieni Mtwara Mjini mpya yenye maendeleo na mafanikio mengi kuanzia sekta ya afya, elimu, maji,shughuli za ujasiriamali, nishati na nyingine nyingi,"amesema Mtenga.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama hao wa CUF ambao wamejiunga CCM wamesema kuwa, wameamua kufanya hivyo kwa madai kuwa,walitafakari kwa kina na kuona kuwa, kwa sasa hamna chama mbadala ambacho kina uwezo wa kushindana na CCM kutokana na namna ambavyo kinatekeleza ilani yake chini ya Dkt.John Magufuli.
 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news