Kocha Cedric Kaze (kulia) ambaye ni raia wa Burundi akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam leo Oktoba 16,2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dkt. Mshindo Msolla, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hatua ya leo inakuja baada ya hivi karibuni Uongozi wa Klabu ya Yanga SC kumfuta kazi kocha wake, Zlatko Krmpotic baada ya makubliano kati ya pande zote mbili.
Yanga SC ilimtakia mafanikio mema sehemu nyingine anayoelekea ambapo Kocha Zlatko alihudumu kwa siku 37 pekee ndani ya klabu ya Yanga SC.