Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Watanzania kumiminika katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kuwachagua madiwani, wabunge na Rais, wagombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Magufuli na Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu wameibuka katika jukwaa la Twitter kuwaomba Watanzania kura, anaripoti Mwandishi Diramakini.
|
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulia na Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu (kushoto) ambao wanaendelea na kampeni za kuwaomba Watanzania ifikapo Oktoba 28, mwaka huu wawape kura ili waweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo kulingana na sera na ilani ya vyama vy |
Aliyeanza kuomba kura kupitia jukwaa hilo ni Rais Dkt.John Magufuli akafuatiwa na Tundu Lissu huku maombi yao yakiwa na mfanano mmoja.