EU yaweka wazi ushirikiano na Uingereza

Umoja wa Ulaya umesema unaendelea kufanyia kazi makubaliano mapya ya Uingereza kujiondoa katika umoja huo maarufu kama Brexit na kutupilia mbali kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, kuwa wako tayari kuondoka bila makubaliano, kauli ambayo imeelezwa kuwa haina mashiko, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais wa Halmshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen. (Francois Walschaerts/EPA).

Rais wa Halmshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amesema baada ya kauli ya Waziri Mkuu Boris Johnson kwamba umoja huo unaendelea kufanyia kazi makubaliano na kusisitiza kwamba hilo halifanyiki kwa gharama yoyote.

Katika ujumbe aliouweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Ursula von der Leyen amesema, timu yao ya majadiliano itakwenda jijini London wiki ijayo kuongeza nguvu katika majadiliano hayo.
Wakati huo huo, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel ambaye ndiye mwenyekiti wa vikao vya wakuu wa mataifa ya kanda hiyo, amerudia maneno hayo wakati wa kuhitimisha mkutano wa siku mbili wa kilele wa viongozi wakuu wa serikali na mataifa ya Umoja wa Ulaya, akisema wameungana na wamedhamiria kuwezesha kufikiwa kwa makubaliano hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news