Leo Oktoba 17, 2020 Serikali mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimetia saini makubaliano ya kuondoa hoja tano za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Sherehe hizo zimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam huku akiwakilisha timu iliyotia saini makubaliano hayo katika sherehe zilizohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali mbili ikiwemo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya Muungano wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu ameyataja mambo hayo kuwa ni ushirikishwaji wa SMZ katika masuala ya Kimataifa na kikanda.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar,Issa Haji Gafu wakitia saini Hati za Makubaliano ya kuondoa hoja tano za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi ikiwemo ushirikishwaji wa SMZ kwenye masuala ya Kimataifa na Kikanda, hafla iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi iliyofanyika leo Oktoba 17,2020 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akilihitubia Taifa kwa njia ya Televisheni na Redio kwenye kikao cha utiaji saini hati za makubaliano ya kuondoa Hoja za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi, ambapo hoja tano zimeondolewa ikiwemo ushirikishwaji wa SMZ kwenye masuala ya Kimataifa na Kikanda na Biashara, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Bara,Dkt. Alan Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee wakibadilishana Hati za Makubaliano ya kuondoa hoja za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi kuhusu uandaaji vikao vya pamoja muda mfupi baada ya kusaini Hati hizo katika Hafla iliyoshudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhun Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo Octoba 17,2020 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Waziri wa Biashara Viwanda na Uwekezaji Mhe. Inocent Bachungwa kushoto na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali wakibadilishana Hati za makubaliano ya kuondoa Baadhi ya Hoja za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi kuhusu Biashara muda mfupi baada ya kusaini Hati hizo katika Hafla iliyoshudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhun Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo Octoba 17,2020 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam.
Waziri Zungu amesema pia kuna. ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, gharama ya kushusha mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar, utafutaji na uchimbaji wa mafuta ya gesi asilia na utaratibu wa vikao vya Kamati ya Pamoja ya Kushughulikia Masuala ya Muungano.

Pia Waziri Zungu amesema, hatua hiyo imechangiwa na kikao cha
kamati ya pamoja ya kushughulikia masuala ya Muungano kuridhia
kuondolewa hoja hizo tano za muungano zilizopatiwa ufumbuzi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha miaka mitano wamefanikisha dhamira kwa vitendo katika kuimarisha muungano. Amesema, Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa mchango mkubwa katika mafanikio hayo.