Ikulu yataka Alexei Navalny apuuzwe

Oktoba 1,2020 Ikulu ya Urusi (Kremlin) imekanusha madai yaliyotolewa na kiongozi wa upinzani nchini humo, Alexei Navalny kuwa Rais Vladimir Putin alihusika na shambulizi hatari la kiambata cha sumu dhidi yake.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov amesema Serikali mjini Moscow inaziyazingatia madai ya Navalny dhidi ya Rais Putin kuwa yasiyo na msingi na hayakubaliki kwa namna moja au nyingine.

Aidha,kupitia taarifa iliyotolewa na Shirika la habari la Urusi, Msemaji Peskov pia amemtuhumu Navalvy kuwa kibaraka wa Shirika la Ujajusi la Marekani (CIA).

Peskov amesema, si mara ya kwanza kwa
shirika hilo kumtumia mwanasiasa huyo kwa maslahi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news