Joyce Sokombi wa NCCR Mageuzi aahidi kuanzisha mfuko maalum kusaidia jamii Musoma Mjini

Mgombea Ubunge kupitia Chama cha NCCR Mageuzi Jimbo la Musoma Mjini, Joyce Sokombi amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ataanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia makundi maalumu katika kata za Manispaa ya Musoma ikiwemo wazee na walemavu,anaripoti Amos Lufungulo (Diramakini) Mara.

Amesema hayo akiwa katika kampeni za kunadi sera na kuomba kura kwa wananchi wa Kata ya Iringo Manispaa ya Musoma, ambapo amesema lengo la kuanziasha mfuko huo, ni kuyawezesha makundi hayo kumudu mahitaji yao ya kila siku ikiwemo matibabu tofauti na sasa.Joyce Sokombi akiwasili eneo la Iringo pembeni yake wakiwa ni Walinzi wake, amefanya Mkutano wa Kuomba kura katika kata ya Iringo Musoma Mjini.(Diramakini).Mgombea Ubunge Kupitia NCCR Mageuzi Jimbo la Musoma Mjini Joyce Sokombi (katikati)akiwasili eneo la Mkutano wa kampeni zilizofanyika Iringo Manispaa ya Musoma. (Diramakini).Mgombea Ubunge Kupitia NCCR Mageuzi Jimbo la Musoma Mjini, Joyce Sokombi akihutubia wananchi katika eneo la mkutano wa kampeni zilizofanyika Iringo Manispaa ya Musoma. (Diramakini).

Sokombi ameahidi kuwezesha ujenzi wa shule ya sekondari ndani ya eneo la Kata ya Iringo kwa lengo la kuwaondolea adha wanafunzi wa kata hiyo, ambao kwa sasa wanasoma katika Shule ya Sekondari ya Nyabisare iliyopo Mtaa wa Nyabisare Kata ya Bweri umbali mrefu kutoka katika kata hiyo.

"Nitatafuta eneo ndani ya kata ya Iringo kuwezesha ujenzi wa sekondari, hii pia itaimarisha usalama wa wanafunzi wetu wa kike kusoma kwa ufanisi,wakati mwingine mabinti zetu huingia kwenye vishawishi vya kimapenzi kwa kusoma mbali na eneo lao na kukosa usimamizi wa karibu,na nitahakikisha pia nawezesha ujenzi wa bweni kusudi adha ya kutembea kwenda Nyabisare waondokane nayo naombeni mnichague niyafanye haya,"amesema Sokombi.

Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya Iringo, Neema Athumany na Yusta Zephania wamesema kwa nyakati tofauti kuwa, watafurahi endapo Sokombi atashinda na kuweza kutekeleza ahadi yake aliyoahidi ya kujenga sekondari ndani ya kata hiyo,wamesema wanafunzi wa kike wataweza kusoma kwa ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news