Katibu Mkuu CCM ana kwa ana na Mabalozi mbalimbali leo


Picha hii iliyopigwa katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva nchini Uswisi na Jean-Marc Ferré wa UN,isikusumbue. Hoja ni kukupa taswira halisi ya baadhi ya bendera za Mataifa mbalimbali Duniani ambayo yana mabalozi wake hapa nchini ambao leo Oktoba 15, 2020 wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Bashiru Ally Kakurwa jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Leo Oktoba 15, 2020, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, atakutana na kufanya mazungumzo na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoonwa na Mwandishi Diramakini, mazungumzo hayo yatafanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Lumumba jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne leo. Hili kujua kitakachojiri endelea kufuatilia hapa kwa taarifa zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news