Kim Jong Un aja kwa sura tofauti

Siku moja baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea kujaribisha miongoni mwa makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kuvuka bara moja kwenda bara lingine, Korea Kusini imeitaka Korea kuonesha nia halisi ya ahadi zake za awali za kuondoa silaha hizo hatari, anaripoti Mwandishi Diramakini (Mashirika).

Katika gwaride la Kijeshi ambalo lilikaguliwa na Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 75 tangu kuasisiwa chama tawala mjini Pyongyang Jumamosi,taifa hilo lilionesha aina mbalimbali za mifumo ya silaha.

Miongoni mwa silaha hizo ni makombora mawili ambayo yameoneshwa hadharani kwa mara ya kwanza kwa mataifa ya nje licha ya jitihada mbalimbali zinazoendelea za kutaka usitishwaji wa urutubishwaji wa silaha hizo. ICBM ni kati ya makombora yanayotajwa kuwa hatari zaidi ambalo linavuka mipaka ya bara lingine huku nyambizi ikitegemewa katika kulifyatua.

Serikali ya Korea Kusini kupitia Wizara ya Ulinzi imeonyesha wasiwasi juu ya hatua hiyo ya Korea Kaskazini.Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo imeitaka Korea Kaskazini kuendelea kuwa sehemu ya makubaliano ya pamoja ya Korea ya mwaka 2018 yenye lengo la kupunguza uadui baina pande hizo mbili.Zinazofanana hapa.

Pia Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini imetoa taarifa tofauti inayoitaka Korea Kaskazini kurejea katika mazungumzo ili kupiga hatua katika nia yake thabiti ya kufikia kutokuwa na silaha za kinyuklia na amani katika Rasi ya Korea, jambo ambalo ni tamanio la kila mwananchi na Dunia kwa ujumla.

Aidha, baada ya mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Taifa, wajumbe wa baraza hilo nchini Korea Kusini wamesema wataendelea kufanya tathmini ya umuhimu wa mkakati wa mfumo wa silaha wa Korea Kaskazini uliooneshwa ikiwemo kufanya mapitio mapya ya uwezo wa ulinzi katika taifa hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news