KMC FC yatuma salamu kwa Polisi Tanzania FC

Kikosi cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) kimetuma salamu kwa Timu ya Polisi Tanzania kuwa wajipange kwa mchezo wa kesho kwani wanazawadi ambayo wamewaandalia,anaripoti Christina Mwagala (KMC FC).

Kesho kikosi hicho kinachonolewa na kocha mzawa Habibu Kondo kitashuka dimbani kuwavaa Polisi Tanzania ikiwa ni wenyeji wa mchezo huo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

KMC FC imetamba kuwafunga wapinzani wao kutokana na kufanya mazoezi ya kutosha na kwamba wakotayari kwa ajili ya kuwa kata vipande vipande ili kujiweka katika nafasi nzuri ya msimu wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Kikosi hicho ambacho kimekuwa kikifanya vizuri katika msimu huo wa Ligi Kuu Tanzania kimejipanga vizuri na kwamba hakuna mchezaji mwenye majeraha na hivyo kikotayari kupambania ushindi hapo kesho na hivyo kuibuka na pointi tatu muhimu.

"Kikosi chetu kipo vizuri, Polisi Tanzania wajiandae kwani mchezo wa kesho utakwenda kuturudisha kwenye kasi ya mchezo wa kutokufungwa kila mechi, na hivyo kuwapa furaha mashabiki wetu".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news