Mwandishi Diramakini anakuletea mkusanyiko wa matokeo yote ya wabunge wateule kutoka kila kona ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kadri yanavyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi, Endelea...
Picha kwa hisani ya LeoTz |
MOSHI VIJIJINI
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrick Ndakidemi ametangazwa kuwa Mbunge mteule kwa kutwaa kura 53,891 huku Mgombea wa NCCR Mageuzi, Anthony Komu akipata kura 3,888 akifuatiwa na Ally Shaban wa ACT WAZALENDO kura 3,189.
JIMBO LA KILWA KASKAZINI
Katikaka Jimbo la Kilwa Kaskazini,Francis Ndulane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametangazwa kuwa mbunge mteule kwa kura 20,501 huku Vedasto Nyombali wa CUF akipata kura 8,513.
JIMBO LA BUSANDA
Kwa upande wa Jimbo la Busanda mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Magesa Bryceson Tumaini ameibuka mnunge mteule kwa kura 50,412 akifuatiwa na Masanja Mihalalo Kapalatu wa CHADEMA kwa kura 11,635 huku Kinasa Tumaini wa ACT-WAZALENDO akipata kura 1,785.
JIMBO LA MPWAPWA
Wakti huo huo CCM wilayani Mpwapwa imeongoza kwa asilimia 100 katika uchaguzi Mkuu wa wa wabunge na madiwani.
Mimamizi wa Uchaguzi wa majimbo ya Mpwapwa na Kibakwe, Sweya Mamba amesema, kwa jimbo la Mpwapwa kulikuwa na kata 15 ambapo kata zote za Jimbo la Mpwapwa wagombea wote wa CCM waliongoza katika uchaguzi huo.
Mamba amesema kuwa, kwa jimbo la Kibakwe pia kulikuwa na kata 18 ambapo kata zote zimechukuliwa na Chama Cha Mapinduzi na kata sita wagombea walipita bila kupigwa.
Msimamizi amesema, nafasi ya ubunge kwa Jimbo la Mpwapwa, Nathan Malima ameongoza kwa kura 29,623 sawa na asilimia 83.12 kati ya kura 4,1621 zilizopigwa ambapo alidai mgombea wa CHADEMA,Ezekiel Chisinjila amepata kura 5,989 Sawa na asilimia 16.88.
JIMBO LA KIBAKWE
Katika hatua nyingine, ChamaCha Mapinduzi (CCM) kimetwaa tena Jimbo la Kibakwe kupitia George Simbachawene ambaye ameapta kura 37,626 Sawa na asilimia 90 na mgombea wa Chadema alipata kura 3,072.
JIMBO LA MWANGA
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mwanga, Zefrin Lubuva amemtangaza Mgombea Ubunge Jimbo la Mwanga, Joseph Anania kupitia CCM kuwa mshindi kwa kura 27,127 na kufuatiwa na Henry John wa CHADEMA kwa kura 4,128.
JIMBO LA CHATO
Katika Jimbo la Chato mkoani Geita Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Dkt.Medard Kaleman kimetwaa tena Jimbo hilo kwa kura 135,999 huku Lucas Mtabi wa CHADEMA akipata kura 7,473.
JIMBO LA GEITA
Katika Jimbo la Geita mkoani Geita, Joseph Kasheku Musukuma wa CCM ameoata kura 31,520 huku mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Neema Steven Chozaile akipata kura 3,901.
JIMBO LA RUANGWA
Katika hatua nyingine Mbunge mteule wa Jimbo la Ruangwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amepokea cheti cha kumtambulisha rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.
Amepokea cheti hicho Oktoba 29, 2020 kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Ruangwa, Bw. Frank Chonya katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Akizungumza mara baada ya kupokea cheti hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema anamshukuru Mungu kwa kuwezesha yote na kuwafikisha hapo na kuwavusha salama kipindi cha kampeni kwa karibu miezi miwili.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye alikuwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, alisema kipekee anashukuru vyama vya siasa wilayani humo kwa kumuamini na kuthamini maendeleo. "Sisiti kusema vyama vya siasa vimeendelea kuthamini maendeleo ya wilaya yetu. Lakini katika hili, niseme kwamba tumeliweka mbele sana suala la maendeleo ya wilaya yetu. Ninawashukuru sana."
Amesema kupatiwa cheti cha kumtambua rasmi kuwa mbunge mteule hadi atakapoapishwa, kumetokana na imani yao kubwa waliyoionesha kwake na kuamua apite bila kupingwa.
"Leo niko hapa mbele yenu, nimemaliza muda wangu wa 2015-2020, mmenivumilia, mmenipa ushirikiano na mmenisaidia kuifanya kazi yangu vizuri. Ninawashukuru viongozi wote na wananchi wa Ruangwa kwa mchango wenu uliowezesha Ruangwa ipige hatua ya maendeleo. Mimi, mke wangu na watoto tunawashukuru sana."
Amesema katika miaka mitano iliyopita, yako mambo mengi waliyofanya na katika kipindi hiki yako mambo yaliyobakia kama kupeleka umeme na maji vijijini. "Ninawaahidi kushirikiana nanyi ili kufikia malengo yaliyowekwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM."
Aliwapongeza madiwani wote walioshinda katika kata zote 22 na kuwaahidi kuwa yuko pamoja nao kuijenga Ruangwa.
Mapema, akizungumza kabla ya kumkabidhi cheti chake, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Ruangwa, Bw. Frank Chonya alisema jimbo hilo lenye kata 22, lilikuwa na watu waliojiandikisha kupiga kura 106,043 na lilikuwa na vituo 311 vya kupigia kura.
Alisema vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo ni CCM, ACT Wazalendo, CUF na CHADEMA. "Kabla ya uchaguzi, kata saba, wagombea wake kutoka Chama cha Mapinduzi walipita bila kupingwa. Jana baada ya uchaguzi, CCM imeshinda kata 12, ACT kata mbili na CUF kata moja."
JIMBO LA KARAGWE
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Karagwe na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe, Godwin M. Kitonka amemtangaza
Mgombea ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa kuwa mshindi wa Ubunge
jimbo la Karagwe katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020 wa kumchagua
Rais, Wabunge na Madiwani.
Jimbo la Uchaguzi Wilaya ya Karagwe lilikuwa na Wagombea wawili kwa nafasi za ubunge ambao ni Ndugu Innocent Lugha Bashungwa kutoka Chama Cha Mapinduzi na Ndugu Adolf Peleus Mkono kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Jumla ya kura zilizizopigwa ni 85,922, kura zilizoharibika ni 1,788, kura halali ni 84,144. Ndugu Adolf Peleus Mkono kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepata kura 15,773 ambayo ni sawa na asilimia 18.35 ya kura halali na Ndugu Innocent Lugha Bashungwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) amepata kura 68,371 ambayo ni sawa na asilimia 81.254 ya kura halali.
JIMBO LA NKASI KASKAZINI
Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Akson ameibuka mshindi katika uchaguzi wa eneo hilo.
Dkt.Tulia Akson alimshinda Sugu kwa kura 75,225 dhidi ya kura 37,591 za Joseph Mbilinyi. Hivyo, Dkt.Tulia kutangazwa kuwa Mbunge mteule wa Mbeya Mjini.
Mgombe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametangazwa kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Arusha Mjini.
Ni baada ya Godbless
Lema wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kutetea jimbo lake la Arusha Mjini, baada ya
kushindwa na mgombea wa CCM, Mrisho Gambo aliyepata kura 82,480 huku
Lema akiwa na kura 46,489, Lema amekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka 10 jimboni humo.
Wakati matokeo ya uchaguzi yanaendelea kutolewa hapa katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, 2020 kuna baadhi ya wagombea waliopita bila kupigwa.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania, ilitoa taarifa siku za nyuma kwa umma kuhusu kuteuliwa kwa wagombea pekee wa ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Wagombea hao ni kutoka majimbo 18 kati ya majimbo 264 ambayo wagombea walikuwa wameingia kwenye kinyang'anyiro.
Job Ndugai
Job Ndugai kutoka jimbo la Kongwa. Bwana Ndugai alikuwa spika wa Bunge la 11 la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.Bwana Ndugai alikuwa Spika wa 7 wa Bunge la Tanzania tangu uhuru.
Profesa Palamagamba
Profesa Palamagamba wa CCM katika jimbo a Kilosa alikuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania katika serikali ya iliyopita.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Kabudi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Dkt. Hamisi Kigwangalla
Dkt. Hamisi Kigwangalla amepita bila kupingwa kupitia chama cha Nzega mjini na mara ya kwanza anaingia Bunge alikuwa miongoni mwa wanasiasa vijana akiwakilisha Nzega eneo la Tabora.
Pia aliwahi kukamatwa na maafisa wa uhamiaji kwa mdai kwamba sio raia wa Tanzania na hilo likawa gumzo kwenye vyombo vya habari Tanzania. Dkt. Kigwangalla alichaguliwa tena mwaka 2015.
January Makamba
Mwingine ni January Makamba wa Bumbuli aliyekua Waziri ofisi ya makamu wa rais ambaye aligombea tena Ubunge katika jimbo la Bumbuli -Tanga katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kuna wakati Januari Makamba alidaiwa kuwa miongoni mwa viongozi ambao sauti zao zilisikika mitandaoni zikimzungumzia vibaya rais Magufuli.
Lakini Rais Magufuli akakiri kumsamehe.
Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa. Alikuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa tangu mwaka 2010 akigombea kwa CCM.
Tarehe 19 Novemba 2015 Bwana Majaliwa aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania.
Aliwahi kushika vyeo vya naibu waziri wa utawala wa mikoa na serikali ya mitaa katika ofisi ya waziri mkuu tangu mwaka 2010 na mkuu wa mkoa wa Lindi kuanzia 2006 hadi 2010.
Bwana majaaliwa ni mpenzi wa michezo ya klabu za Tanzania na ni shabiki wa Simba S.C.
Wengine waliopita moja kwa moja ni pamoja na:
- Mhandisi Isaack Kamwelwe wa Mlele
- Elias Kwandikwa Jimbo la Ushetu,
- Philipo Augustino Mulugo wa Songwe
- Zedi Jumanne wa Bukene
- Ahmed Shabiby jimbo la Gairo
- Jonas Van Zeela wa Mvomero
- Nape Nnauye wa Mtama
- Kalogereris Innocent wa Morogoro Kusini
- Vita Rashid Mfaume Kawawa wa jimbo la Namtumbo
- Taletale Hamis Shabani wa Morogoro Mashariki
- Jumanne Sagini wa Butiama
- Alexander Mnyeti jimbo la Misungwi
- Geofrey Pinda wa Kavuu
Mgombea wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga Ahmed Salum (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020 baada ya kupata kura 68,066 akifuatiwa na Washington Kasonzo (CHADEMA) aliyepata kura 11,785, Aloyce Shija (CUF) kura 1,111 na Leonard Kitile (NCCR – Mageuzi) kura 526.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Solwa, Hoja Mahiba amesema waliondikishwa kupira kura katika jimbo la Solwa ni 190,962,waliopiga kura ni 83,040,kura halali ni 81,488 na kura zilizoharibika ni 1552.
JIMBO LA MAKETE
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Makete, amemtangaza Mgombea Ubunge jimbo hilo Kupitia (CCM) Festo Sanga kuwa mshindi kwa kupata kura 24,237 akifuatiwa na Ahadi Mtweve (CHADEMA) mwenye kura 5077 na Grace Jekela (NCCR) kura 981.
JIMBO LA MBAGALA
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbagala, Lusubilo Mwakabibi, amemtangaza Mgombea Ubunge Jimbo hilo Kupitia CCM Abdallah Chaurembo kuwa mshindi kwa kupata kura 283,000 akifuatiwa na Hadija Mwago (CHADEMA) mwenye kura 13,985 na Kondo Bungo (ACT) kura 3856.
Msanii Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amefanikiwa kushinda nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Muheza,Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimshinda mpinzani wake Yosepher Komba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, amemtangaza Mwana Fa wa CCM kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa jimbo hilo baada ya kupata kura 47,578 na kumshinda Yosepher Komba wa CHADEMA aliyepata kura 12,034.
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
Waliojiandikisha ni 118,430, waliopiga kura 55,049, kura halisi 53,271 sawa na asilimia 100, kura zilizo haribika ni 1,778.
Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF),Shemsia Mtamba ametangazwa kuwa Mbunge Mteule Jimbo la Mtwara Vijijini ni baada ya kumshinda Hawa Ghasia, mmoja wa vigogo na aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya Taznania kwa vipindi tofauti.
Shamsia Mtamba wa Chama cha Wananchi (CUF) ameibuka kidedea kwa kura 26,262 mbele ya Hawa Ghasia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 18,505.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, Emmanuel J. Mkongo, kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 81 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 rejeo la 2015 na kanuni ya 69(1)(d) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za Mwaka 2020, amemtangaza Dkt.John Danielson Pallangyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa nafasi ya kiti cha Ubunge jimboni humo kwa kupata kura nyingi zaidi dhidi ya Bi. Rebecca Michael Mgondo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Tarehe 28 Octoba 2020.
Dkt.John D. Pallangyo amepata kura 84,858 na Bi.Rebecah Michael Mgondo amepata kura 14,688 ikiwa idadi ya wapiga kura walioandikishwa ni194,367 idadi ya waliopiga kura 100,885, kura halali 99,458 na kura zilizokataliwa ni 1427.
Aidha, Msimamizi huyo wa uchaguzi amemkabidhi Dkt.John D. Pallangyo cheti cha ushindi wa nafasi ya Kiti cha Ubunge.Ikumbukwe kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa na wagombea toka vyama viwili tu CCM na CHADEMA.
Katika uchaguzi huu Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa na vituo 521 vya kupiga kura katika Kata 26.Pia idadi ya wapiga kura walioandikishwa jimboni humo ilikua 194 ,367.
Aidha Kata 20 pekee ndio zilizo kuwa na uchaguzi wa Madiwani kwani Kata 6 zilizobakia wagombea wake walipita bila kupingwa wakati wa zoezi la awali la uteuzi wa Wagombea.
Baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika katika vituo vya kupiga kura wagombea watokanao na Chama cha Mapindizi (CCM) wameongoza katika kata zote 20 zilizokuwa na uchaguzi wa Madiwani hivyo kupelekea Chama hicho kuongoza katika Kata zote 26.
Katika Jimbo la Ngorongoro Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea kupitia mgombea wake, William Ole Nasha aliyepata kura 63,536 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Jaquelin Swai kikipata kura 7982.
Eric James Shigongo ametimiza ndoto baada ya kutangazwa mshindi na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buchosa mkoani Mwanza, Crispine Luanda.
Pia wagombea udiwani wa kata za Jimbo la Buchosa kupitia CCM wametangazwa kushinda wote 21 kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28,mwaka huu.
Luanda amesema, Shigongo amepata kura 79,950 na kuwashinda wapinzani wake Mayla Elia wa CHADEMA aliyepata kura 11,285 huku Richard Preade wa ACT Wazalendo akipata kura 937.
Shigongo alianza kuliwinda Jimbo la Buchosa mwaka 2010 na 2015 akichuana vikali na Dkt. Charles Tizeba kwenye mchakato wa ndani ya CCM ambapo mara mbili kura hazikutosha ambapo mwaka huu kwenye mchakato wa ndani wa CCM, Shigongo na Dkt. Tizeba walipata kura 334, lakini kwa vile Dkt.Tizeba alikuwa mpiga kura iliondolewa kura moja ambayo ilimpa fursa Shigongo ya kuwa mgombea wa CCM Jimbo la Buchosa.
JIMBO LA SENGEREMA
Katika Jimbo la Sengerema, Hamis Mwagao Tabasamu wa CCM ametangazwa mshindi wa jimbo hilo kwa kura akimshinda mpinzani wake wa karibu.
Jimbo la Sengerema kwa vipindi vitatu lilikuwa likishikiliwa na William Ngeleja, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini wakati huo ambaye naye alilirithi kutoka kwa Dkt. William Shija (marehemu).
Itakumbukwa Tabasamu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aliwania jimbo hilo kupitia CHADEMA akashindwa na Ngeleja kabla ya kurejea CCM.
JIMBO LA MAGU
Katika hatua nyingine, wagombea Ubunge wa Majimbo ya Magu na Kwimba wote CCM, Boniventura Kiswaga na Shanif Mansoor, wamefanikiwa kutetea viti vyao baada ya kuwabwaga wapinzani wao kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Pia CCM imetwaa Jimbo la Sumve baada ya mgombea wake Kasalali Emmanuel Mageni kumbwaga mshindani wake wa karibu Salagani Shija Masanja wa CHADEMA.
MAGU
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Magu, Lutengano Mwalwiba akitangaza matokeo ya uchaguzi huo kwenye jimbo hilo alisema lilikuwa na wapiga kura 190,026 na vituo 540.
Amesema, vyama vilivyosimamisha wagombea kwenye uchaguzi huo ni vitatu na kuvitaja kuwa ni CCM,CHADEMA na ACT Wazalendo.
Msimamizi huyo wa Uchaguzi Jimbo la Magu amesema, kura zilizopigwa ni 158,106 , zilizoharibika 699 ambapo Kiswaga alipata kura 139,975 sawa na asilimia 88.9 na kumwacha mpinzani wake wa karibu,Reginald Kwizera wa CHADEMA kura 14,479.
Kwa mujibu wa msimamizi huyo kura za Urais mgombea wa CCM alikuwa akiongoza kwa 171,679 sawa na asilimia 93.27 akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu kwa kura 10,840.
JIMBO LA KWIMBA
Katika Jimbo la Kwimba, Msimamizi wa Uchaguzi, Pendo Malabeja amesema katika jimbo hilo watu 170,671 walijiandikisha kupiga kura ambapo waliopiga ni 61,632 na kura 849 ziliharibika.
Amesema, kwenye uchaguzi mkuu huo wa mwaka huu vyama vya CCM, CUF na Demokrasia Makini vilisimamisha wagombea wao.
Malabeja amemtangaza mgombea wa CCM, Shanif Mansoor kuwa mshindi baada ya kupata kura 57,943 na kuwabwaga wapinzani wake Joseph Kayanda wa CUF kura 1,917 na Mayeka Kabwe wa Demokrasia Makini kura 923.
Hata hivyo kwenye viti vya udiwani CCM imechukua viti 13 kati ya 15 vya Jimbo la Kwimba na kupoteza kata mbili zilizoangukia mikononi mwa CHADEMA.
JIMBO LA SUMVE
Kwa upande wa Jimbo la Sumve,Kasalali Emmanuel Mageni wa CCM amepata kura 31,373 kati ya 38,380 zilizopigwa na kuwaangusha, Salagani Shija Masanja wa CHADEMA aliyepata kura 6,285 na Joseph Steven Madelehe wa CUF aliyepata kura 722.
Malabeja amemtangaza Kasalali kuwa mshindi wa ubunge kwenye Jimbo la Sumve lililokuwa likishikiliwa na marehemu Richard Ndasa kwa vipindi vitatu.
Kwa mujibu wa Msimamizi huyo wa uchaguzi Jimbo la Sumve lilikuwa na wapiga kura 94,029 kati ya hao waliojitokeza kupiga kura ni 39,715 ambapo kura 1,335 ziliharibika na kufanya kura halali kuwa 38,380 huku CCM pia ikizoa viti 15 vya udiwani kwenye jimbo hilo.
Mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Busega pamoja na Madiwani wametangazwa hii leo tarehe 29/10/2020. Matokeo ya nafasi hizo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Busega Anderson N. Kabuko.
Nafasi ya Ubunge Jimbo la Busega iliwaniwa na wagombea wanne (4) kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ACT Wazalendo na Civic United Front (CUF)
Kura zilizopigwa ni 48,230, kura halali zikiwa ni 46,634, kura zilizoharibika zikiwa ni 1,596, huku jumla ya idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ikiwa ni 124,316. Nafasi ya kiti cha Ubunge imechukuliwa na Simon Songe Lusengekile kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 35,770, akifuatiwa na Adam Alphonce Komanya kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura 9,063.
Kwa upande wa nafasi za kiti cha Udiwani kutoka katika kata 15 zilizopo Jimbo la Busega, CCM imeshinda jumla ya kata 14 huku CHADEMA ikishinda kata moja.
Aidha Kabuko amevishukuru vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na wananchi kwa ujumla kwa kuonesha utulivu kwa kipindi chote cha uchaguzi. Uchaguzi mkuu Jimbo la Busega umefanyika huku hali ya usalama ikiwa shwari, hali iliyopelekea utulivu wa wananchi.
JIMBO LA KASULU MJINI
Kwa upande wa Jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma waliojiandikisha ni 117, 228,waliopiga kura ni 56 , 449 kupitia kura hizo Mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF),Vedasto Magyane amepata kura 317, Vides Kihoza wa NCCR Mageuzi amepata kura 528,Rubibi Kasimu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepata kura 1,510,Hamza Mtundu wa ACT Wazalendo kura 3653 huku Joyce Ndalichako kupitia Chama Chama Mapinduzi (CCM) akipata kura 49,390. Kwa matokeo hayo Profesa Joyce Ndalichako ndiye aliyetangazwa Mbunge Mteule.
Matokeo jimbo la Muhambwe, Kibondo Kigoma
waliojiandikisha 127766
waliopiga kura 50, 180
Atashasta Nditiye 29837 CCM
Felix Mkosamali 15248 Chadema
Julias Makosa 2996 ACT
Nicholus Cosmas 473 CUF
Kura zilizoharibika 1626
Jimbo la Kigoma Kusini
Msimamizi wa Uchaguzi Weja Ng´olo
1.Nuru Bashange UMD 157
2. Daniely Ntaondenga ADA TADEA 297
3. Ahmad Machali CCK 438
4. Ibrahim Ntagalugwa CUF 548
5. Evarist Gregory CHADEMA 2476
6. Hussen Masanga NCCR MAGEUZI 4380
7. Said Rashid ACT 17,222
8. Nashon Bidyanguze CCM 36,496
Waliopiga kura 63,463
idadi ya kura halali 62,014
Jimbo la Buyungu
Msimamizi Masumbuko Stephano
kura zilizopigwa 42, 765
kura halali 41,588
zilizoharibika 1177
1. Aloyce Kamamba CCM 28, 912
2. Ashura Mashaka Chadema 11,602
3. Haruna Balola ACT 801
4. Audax Gasper 181
Jimbo la Kasulu Vijijini
Msimamzi Joseph Ka
Waliojiandikisha 164,285
Waliopiga kura 71,741
Kura Halali 69,792
zilizoharibika 1949
1. Vuma Agustino CCM 37,795
2. Simon Ruseba Chadema 29,904
3. Kazara Kinyoma ACT 9757
4. Pius Msongwa NCCR Mageuzi 947
5. Dickson Batega CUF 389
Jimbo la Kigoma Kaskazini
Msimamizi Pendo Mangali
waliojiandikisha 119418
waliopiga kura 55,565
kura halali 54122
zilizokataliwa 1443
1. Makanika Nelson CCM 24,066
2. Kiza Mayeye CUF 16,252
3. Swage Swage ACT 10,455
4. Akrani Peter CHADEMA 2588
Jimbo la Kigoma Mjini
Msimamizi Mwailwa Pangani
Waliojiandikisha 124,365
waliopiga 50, 268
Kura Halali 50,268
1. Kirumbe Ng´enda CCM 27,688
2. Zitto Kabwe ACT 20,600
3. Magu Zafiri Chadema 1227