Leo Oktoba 17, 2020 Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wamemenyana na Mlandege FC katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamanzi wilayani Temeke, Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katika mechi hiyo, mshambuliaji Mkongo, Chris Mugalu ameifungia Simba SC mabao mawili 8' na 68' huku Ame Ali akipachika bao lingine 16'.Hadi mechi inamalizika kipindi cha kwanza Simba SC ilikuwa kiongoza kwa mabao mawili huku Mlandege FC ikiwa haijapata kitu. Katika kipindi cha pili Yahya Haji wa Mlandege aliipatia timu yake bao 72' ambalo lilikuwa la kwanza na la mwisho.