Ni Oktoba 3,2020 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni raundi ya tano, mechi nne zinapigwa viwanja vinne tofauti kusaka alama tatu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Gwambina vs Ihefu,kuanzia saa 8:00 mchana, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza umeitimika kwa ushindi wa kwanza kwa Gwambina.
Vijana hao wa Misungwi huu ni ushindi wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi nne bila faida.
Meshack Abraham 33' na 48' ndiye aliyepeleka kilio Ihefu FC.
Mchezo uliopita Ihefu FC iliacha alama tatu mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex.
Gwambina FC inafikisha jumla ya alama nne huku Ihefu FC ikibakiwa na alama tatu kwa kuwa ilishinda mchezo mmoja mbele ya Ruvu Shooting.
Namungo VS Mwadui FC
Namungo vs Mwadui FC imeanza saa 10:00 joni, Uwanja wa Majaliwa mjini Lindi.
Namungo FC imepoteza mechi ya pili msimu huu nyumbani baada ya kuchapwa 1-0 na Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa Ruangwa mkoani Lindi.
Namungo FC imezamishwa na Ismail Ally 7' na kwa ujumla huo unakuwa mchezo wa tatu msimu huu Namungo FC inapoteza ndani ya mechi tano.
Mbeya City vs Tanzania Prisons
Pia Mbeya City vs Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine imechezwa kuanzia saa 10:00.
Mbeya City wamelazimishwa sare ya bila kufungana na ndugu zao, Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine jijini humo.
Yanga vs Coastal Union
Yanga vs Coastal Union, majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Yanga SC wapo kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.