Simba SC yaiondoa Yanga SC kileleni kwa 4G

Wekundu wa Msimbazi wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara muda mfupi uliopita kupitia mchuano mkali uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ilikuwa hivi, Simba SC wameichapa mabao 4-0 wenyeji wao JKT Tanzania. Matokeo hayo yanawapa alama 13, baada ya kucheza mechi tano.Wanakwea kileleni kwa kuwazidi wastani wa mabao mahasimu wao, Yanga SC wanaofuatia nafasi ya pili ambao nao jana walikwea katika kilele hicho

Mchezo huo umesimamiwa na Refa Hance Mabena kutoka Tanga aliyesaidiwa na Joseph Masiga wa Mwanza na Geoffrey Msakila wa Geita, hadi mapumziko Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 3-0.

Meddie Kagere 3' yaliwasimamisha mashabiki wa Simba SC baada ya kumalizia kazi nzuri ya Rally Bwalya. Chris Mushimba Kope Mugalu 5' alimalizia kazi nzuri ya Luís Jose Miquissone na kusababisha ukimya kwa JKT Tanzania.

Kagere ndani ya 40' aliweka bao lingine baada ya kumalizia kazi nzuri ya Clatous Chama hadi mapumziko Wekundu wa Msimbazi walikuwa wamejikusanyia mabao matatu kwa sufuri.

Aidha, kipindi cha pili, Luis Jose Miquissone 54' aliongeza shangwe kwa Wekundu wa Msimbazi baada ya kuhitimisha Mfumo wa 4G kwa sufuri dhidi ya JKT Tanzania.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news