Yanga SC wapo kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wanajangwani chini ya Kocha Zlatko Krmpotic inafikisha alama 13 baada ya ushindi huo katika mchezo wa tano leo.Kwa matokeo hayo sasa inaongoza Ligi Kuu kwa alama tatu dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao wana mechi moja mkononi.
Ilikuwa hivi 45' za mchezo huo uliochezeshwa na refa Suleiman Nonga wa Arusha kwa kusaidiwa na Charles Simon na Sunday Komba walizimaliza wakiwa suluhu.
Hata hivyo, baada ya mapumziko Yanga SC walikuja kwa kasi na kuanza kupindua meza.
Mwandishi Diramakini alimshuhudia, Carlos Carlinhos 3' tu kipindi cha pili akifunga bao la kwanza kwa kichwa akimalizia kazi nzuri ya Deus Kaseke aliyechukua nafasi ya beki wa kulia, Kibwana Shomari katika mtanange huo.
Haruna Niyonzima ndani ya 52' alipeleka kilio Coastal Union kwa shuti kali kutoka pembeni ikiwa ni kazi ya Kisinda.
Aidha,Sogne 63' amekamilisha hesabu baada ya kumsomea ramani kipa Ibrahim.Yanga vs Coastal Union, majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.