Wanajangwani wamepata ushindi mwembamba katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC leo Oktoba 9,2020 katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi wilayani Temeke, Dar es Salaam,.
Yanga SC kupitia kwa Michael Sarpong aliyepo katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe klabu ya Jangwani ndani ya 81' alimalizia kazi ya Carlos Carlinhos na kuiwezesha timu yake kuibuka kidedea.Yanga dhidi ya Mwadui FC mchezo wa kirafiki unaochezwa Uwanja wa Azam Complex wilayani Temeke,Dar es Salaam.
Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi alimuanzisha kiungo majeruhi wa muda
mrefu Juma Mahadhi, lakini akampumzisha baada ya 45' ya mchezo.
Yanga SC kilikuwa na Faruk Shikhalo, Kibwana Shomari/Paul Godfrey 88', Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Juma ‘Makapu’, Abdulaziz Makame/Mukoko Tonombe 46', Juma Mahadhi/Carlos Carlinhos 46', Deus Kaseke/Zawadi Mauya 70', Michael Sarpong/Adam Kiondo 88', Waziri Junior na Farid Mussa.
Kwa upande wa Mwadui FC alikuwa ni Mussa Mbisa, Mbarouk Khalfan, Shaaban Kingazi, Abbas Kapombe, Joram Mgeveke, Enrick Nkosi, Wallace Kiango/Salum Chubi 67', Charles Masenga, Deogratius Anthony, Ismail Ally/Msenga Msenga 79' na Freddy Cosmas Lewis hadi mechi hiyo ya kirafiki inakamilika.