Mafuriko yakatisha mawasiliano, yaondoka na madaraja

Wakazi wa mitaa miwili ya Mgeule na Mgeule Juu katika Kata ya Buyuni Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wamelazimika kukosa mawasiliano baada ya madaraja matatu yanayounganisha mitaa hiyo kukatika,ni baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hali iliyopelekea wakazi hao kushindwa kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine kwa ajili ya kufuata huduma za kijamii.

Wamesema, mvua hizo zilizonyesha kwa takribani siku tano mfululizo zimesababisha kukatisha madaraja hayo na hivyo kushindwa kuvuka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine huku hatari zaidi ikiwakumbuka watoto na wanafunzi ambao hulazimika kuvushwa pindi wanapokwenda shuleni.

Aidha, wakazi hao ambao ni Kareem Madenge, Zaina Rashid na Anna Simon wamesema, licha ya kukatika kwa madaraja hayo, lakini pia wakazi wa maeneo hayo wako kwenye hatari ya kuyakimbia makazi yao baada ya nyumba wanazoishi kuzingirwa na maji kufuatia mvua hizo.Tizama video hapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news