Magazeti ya Okaz, Saudi Gazette,Al Madina yajinasua udukuzi wa Kimataifa

Maafisa usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran wanatuhumiwa kutaka kufanya udukuzi wa tovuti za magazeti ya Saudia Arabia ya Okaz na Saudi Gazette. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa magazeti hayo imeeleza kuwa, dhamira ya wadukuzi hao ilikuwa kuchapisha maudhui ambazo zitakwenda kinyume na maadili ili kuyaondolea sifa na heshima magazeti hayo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Taarifa ya uongozi wa magazeti hayo imeongeza kuwa, magazeti hayo yanalengwa kutokana na moja ya machapisho yake ambayo yalikuwa yanaonyesha kuunga mkono Serikali ya Yemen na kupingana na mwelekeo wa Iran.

Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Okaz, Jameel Al-Thiyabi ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Saudi Gazette amesema, wadukuzi hao walilenga kufanya shambulio baya katika tovuti zao ikiwemo kuweka machapisho ambayo yanaonyesha kuunga mkono juhudi za Iran nchini Yemen.

"Kwa ujio huo, kamwe, machapisho yetu hayawezi kubadili ukweli juu ya jambo lolote linalotaka kufanyika Yemen,"amenukuliwa Mhariri Mtendaji huyo huku pia gazeti lingine la Al Madina wakibainisha kuwa,wadukuzi hao walilenga pia tovuti yao.

Saudi Gazette liliasisiwa mwaka 1978 ni kati ya magazeti makubwa nchi Saudi Arabia ambayo huwa yanachapishwa kwa lugha ya Kiingereza huku Okaz likiwa ni gazeti dada.Okaz ni gazeti la Saudi Arabia ambalo huwa linachapishwa kwa lugha ya Kiarabu kila siku mjini Jeddah ambapo liliasisiwa 1960. 

Awali, mashirika ya habari nchini Jamhuri ya Kiislam ya Iran yalikaririwa yakieleza kuwa, matusi ya gazeti la Okaz la Saudi Arabia dhidi ya Wapalestina, ni zaidi ya kuvunja mwiko.

Madai ya vyombo hivyo ni kwamba, katika makala iliyoandikwa na Muhammad al Said wa Okaz hilo kwa madai kuwa, "Wapalestina wametumia ugaidi wa kupanga dhidi ya nchi nyingi za Kiarabu na wametumia bunduki na mabomu yao dhidi ya mataifa ya Waarabu" inapaswa kupuuzwa.

Kwa mujibu wa mashirika hayo, katika miaka ya karibuni Saudi Arabia imedhihirisha waziwazi mienendo yake dhidi ya Palestina, na mfano wa wazi wa ukweli huo ni matamshi yaliyotolewa na mrithi wa ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman Machi, mwaka 2017 huko Marekani.

Wakati huo Bin Salman aliliambia gazeti la Atlantic kwamba: "Saudia ina manufaa mengi na Israel, na kama kutakuwepo amani basi kutapatikana manufaa makubwa baina ya Israel na wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na vilevile na nchi kama Misri na Jordan".

Kwa matamshi yake hayo, mrithi huyo wa kiti cha ufalme cha Saudi Arabia,Jamhuri ya Iran inalalama kuwa, mrithi huyo aliutambua rasmi utawala wa Israel, hivyo wanaiona Saudi Arabia kuwa ni muungaji mkono mkubwa wa mpango wa Marekani wa 'Muamala wa Karne' ambao wanadai lengo lake hasa ni kuiangamiza Palestina.

Pia vyombo hivyo vya Iran vinadai kuwa, Riyadh pia haikuweka wazi msimamo wake kuhusu mpango wa Israel wa kutwaa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na kuyaunganisha na ardhi nyingine zinazokaliwa kwa mabavu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news