MAJALIWA: MAFUNDISHO YA DINI YANACHANGIA AMANI NCHINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally (kulia) na Katibu wa Baraza la Maulamaa, Sheikh Khamis Mataka (kushoto) wakati alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mafundisho na miongozo inayotolewa na viongozi wa dini nchini ndiyo sababu kubwa ya kuifanya Tanzania iendelee kuwa nchi nzuri na yenye amani duniani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally wakifungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Ameyasema hayo Oktoba 10, 2020 baada ya kufungua msikiti wa Rahman uliopo katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Tanga na ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini waendelee kuliombea Taifa.

Waziri Mkuu amesema Watanzania wanatakiwa waendelee kuwarithisha imani za dini watoto wao ili kuwajenga katika misingi mizuri ya maadili itakayowafanya wawe raia wema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe baada ya kuufungua Msikiti huo, Oktoba 10, 2020. Kulia kwake ni Mufti na Sheikh Mkuu waTanzania, Abubakar Zubeir bin Ally. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020. Kushoto ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi wa dini nchini kwa kuliombea Taifa tangu mchakato wa uchaguzi mkuu ulipoanza.

“Tunawashukuru viongozi wa dini, tuna zaidi ya mwezi mmoja tangu kuanza kwa kampeni na bado amani inaendelea kutawala nchini, hivyo msichoke kuliombea Taifa na kuwaombea wote wanaoshiriki katika mchakato wa kampeni.”

Wananchi wa Korogwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Msikiti huo umejengwa kwa gharama ya sh. milioni 150 kwa ufadhili wa taasisi ya Firdausi ambayo imekuwa ikijenge misikiti, kutoa misaada pamoja na kuchimba visima kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Wananchi wa Korogwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa pamoja na wakazi wa Kwamndolwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news