Mshambuliaji wa Manchester United na England, Marcus Rashford (22) amepata tuzo ya heshima ya (MBE) inayotolewa na Malkia wa Uingereza kwa mchango wake alioutoa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Uingereza wakati wa janga la virusi vya corona.
Kampeni ya Mchezaji huyo akishirikiana na serikali iliwezesha watoto karibu milioni 1.3 nchini Uingereza kupata chakula cha bure katika shule mbalimbali wakati wa janga la virusi vya Corona hasa kwenye msimu wa joto.
Rashford amemtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuongeza muda wa mpango huo huku muasisi wa mashindano ya mbio ya 'Great North', Brendan Foster akipata tuzo ya heshima ya Knighthood.
Bingwa huyo wa mbio za mita 10,000 za Jumuia ya Madola, Foster akiiwakilisha England mara tatu kwenye michezo ya Olimpiki kabla ya kuingia kwenye uchambuzi mwaka 1980 alianzisha Great North Run - mashindano makubwa ya ridhaa Uingereza, ikishirikia watu wengi zaidi, kabla ya kuchambua mashindano tisa ya michezo ya olimpiki akiwa na BBC kabla ya kustaafu mwaka 2017.
Aidha, kwenye upande wa mchezo wa raga, kocha mkuu wa zamani wa Wales, Warren Gatland na Gareth Thomas ambaye aliichezea nchi hiyo kwenye mashindano ya ligi na kimataifa amepata tuzo ya CBE, huku Alun Wyn Jones, nahodha wa sasa wa timu hiyo, akipata tuzo ya OBE.
Bingwa mara tatu wa Olimpiki, Eve Muirhead, kutoka Scotland naye amepta tuzo ya MBE, pamoja na nyota aliyetwaa mara 12 mashindano ya Dunia ya snooker kwa wanawake, Reanne Evans na mchezaji wa zamani wa Kriket kutoka England Darren Gough.
Orodha ya tuzo hizo za heshima ya siku ya kuzaliwa kwa Malkia kwa mwaka huu wa 2020, ilitarajiwa kuchapishwa Juni,mwaka huu lakini ilisogezwa mbele ili kuwapa nafasi walioteuliwa kutekeleza majukumu yao muhimu katika miezi ya kwanza hasa ya matatizo.