Hatimaye Nahodha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Mbwana Samatta amewathibitishia wote kwamba ana kipaji zaidi ya wanavyomuuona.
Ni baada ya leo Oktoba 3,2020 kuifungia mabao mawili timu yake ya Fenerbahce katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Karagümrük kwenye Ligi Kuu nchini Uturuki.
Aidha, hii ni mechi ya pili kwa Mbwana Samatta kwenye ligi hiyo ambapo amecheza kwa 84' kabla ya mabadiliko.
Hata hivyo, mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Galatasaray wiki iliyopita ambapo alicheza kwa dakika 25 huku mechi ikimalizika kwa suluhu nchini humo.