Mgombea Urais kupitia NCCR Mageuzi asema baada ya kuapishwa ataanza na miundombinu bora ya elimu

Chama cha NCCR-Mageuzi kimeendelea na ziara zake za kampeni kwenye mikoa mbalimbali nchini Tanzania, lengo likiwa ni kuomba kura kwa wananchi ili kuweza kuunda serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akiwa wilayani Chemba mkoani Dodoma, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Yeremia Kulwa Maganja katika baadhi ya mambo ambayo ameyasemea ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya shule hasa ujenzi wa vyoo bora pamoja na miundombinu wezeshi hasa kwa watoto wa kike kwa ajili ya mahitaji yao.

“NCCR-Mageuzi tutabadili miundombinu ya shule zote. Tutajenga madarasa na vyoo bora na vya uhakika. Ili kuhakikisha wafunzi wa jinsia zote wanakuwa na sehemu maalum kwa ajili ya mahitaji yao,"amesema Yeremia Kulwa Maganja.

Ilani ya chama cha NCCR-Mageuzi kupitia sera ya elimu hasa katika uboreshaji wa mfumo wa elimu 3 (b) 2 inasema Serikali ya NCCR-Mageuzi itaimarisha miundombinu ya shule, hasa maji safi na salama na vyoo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news