Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kutumia shilingi Bilioni 56 kujenga vihenge vya kisasa na maghala ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kufikia tani 501,000 mwaka 2020 toka tani 250,000 mwaka 2015, anaripoti Mwandishi Diramakini (Njombe).
Mgumba amebainisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeweza kusimamia na kutekeleza vyema ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 na kuiwezesha nchi kuwa na uhakika wa chakula kwa kujenga vihenge vya kisasa na maghala.
“Serikali imetumia Shilingi Bilioni 56 kujenga vihenge vya kisasa na maghala katika kanda nane za NFRA ambapo uwezo wa kuhifadhi utaongezeka toka tani 250,000 mwaka 2015 hadi tani 501,000 mwaka 2020,”amesema Mgumba.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, Naibu Waziri Mgumba amesema, Taifa lipo katika hali ya usalama kutokana na uwepo wa utoshelevu wa chakula kufuatia juhudi za wakulima, wafugaji na wavuvi.
“Kwa mujibu wa takwimu za uzalishaji na tathmini iliyofanyika hivi karibuni ya msimu wa 2019/2020, inaonesha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula unatarajia kufikia tani 17,742,388 ambapo mahitaji ni tani 14,347,955,”amesema Naibu Waziri Mgumba.
"Kauli mbiu ya Siku ya Chakula Duniani mwaka huu inasema ‘Kesho Njema Inajengwa na Lishe Bora Endelevu’ ambapo Serikali imedhamiria kutatua changamoto za lishe kwa kuendelea kutekeleza Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe (National Multsectoral Nutrition Action Plan- 2016/2017- 2020/2021) na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDPII)," amesisitiza Mgumba.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya amesema mkoa wake una ziada ya chakula tani 700,000, lakini wanakabiliwa na tatizo la udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano unaofikia asilimia 49.4 mwaka 2019.
Amebainisha kuwa, mkoa wake kupitia maadhimisho haya utaweza kufikisha elimu ya lishe bora kwa wananchi ili kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kuendeleza shughuli za uzalishaji mali.
“Tumepanga kama mkoa kupambana na tatizo la udumavu kwa watoto ili tufikie angalau asilimia 33 toka 49.4 ya sasa kwani Njombe ina vyakula vingi isipokuwa hatuli vema,”amesisitiza Mhadisi Marwa.
Mhandisi Marwa amebainisha kuwa, Mkoa wa Njombe unahitaji wawekezaji wengi kwenye sekta za kilimo,mifugo na uvuvi kutokana na uwepo wa ardhi yenye rutuba na hali ya hewa nzuri.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah amesema sekta hiyo imeendelea kukua na kuchangia asilimia 30 ya protini inayotokana na wanyama na inatoa ajira kwa Watanzania takribani milioni 4.5.
Dkt.Tamatamah ameongeza kuwa, katika mwaka 2019/20, Sekta ya Uvuvi ilikua kwa kiwango cha asilimia 1.5 na kuchangia Pato la Taifa (GDP) kwa asilimia 1.71 ambapo uzalishaji wa samaki kutoka maji ya asili kwa mwaka 2019/20 ulifikia takribani tani 497,567 na katika uzalishaji wa mazao ya viumbe maji kufikia tani 18,716.56.
Mgumba amebainisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeweza kusimamia na kutekeleza vyema ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 na kuiwezesha nchi kuwa na uhakika wa chakula kwa kujenga vihenge vya kisasa na maghala.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Chakula, Dkt.Honest Kessy akitoa salamu za wizara kwa niaba ya Katibu Mkuu Kilimo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa mkoani Njombe. |
|
“Kwa mujibu wa takwimu za uzalishaji na tathmini iliyofanyika hivi karibuni ya msimu wa 2019/2020, inaonesha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula unatarajia kufikia tani 17,742,388 ambapo mahitaji ni tani 14,347,955,”amesema Naibu Waziri Mgumba.
"Kauli mbiu ya Siku ya Chakula Duniani mwaka huu inasema ‘Kesho Njema Inajengwa na Lishe Bora Endelevu’ ambapo Serikali imedhamiria kutatua changamoto za lishe kwa kuendelea kutekeleza Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe (National Multsectoral Nutrition Action Plan- 2016/2017- 2020/2021) na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDPII)," amesisitiza Mgumba.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya amesema mkoa wake una ziada ya chakula tani 700,000, lakini wanakabiliwa na tatizo la udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano unaofikia asilimia 49.4 mwaka 2019.
Amebainisha kuwa, mkoa wake kupitia maadhimisho haya utaweza kufikisha elimu ya lishe bora kwa wananchi ili kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kuendeleza shughuli za uzalishaji mali.
“Tumepanga kama mkoa kupambana na tatizo la udumavu kwa watoto ili tufikie angalau asilimia 33 toka 49.4 ya sasa kwani Njombe ina vyakula vingi isipokuwa hatuli vema,”amesisitiza Mhadisi Marwa.
Mhandisi Marwa amebainisha kuwa, Mkoa wa Njombe unahitaji wawekezaji wengi kwenye sekta za kilimo,mifugo na uvuvi kutokana na uwepo wa ardhi yenye rutuba na hali ya hewa nzuri.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt.Rashid Tamatamah akitoa salamu za wizara yake wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani kitaifa mkoani Njombe. |

Tags
Habari