TANAPA yaongeza nguvu kuukabili moto unaofanananishwa na wanyika Mlima Kilimanjaro

  

Moto huo unadaiwa kutokea pembezoni mwa Mlima Kilimanjaro (Mawenzi). Jitihada za Mwandishi Diramakini kupata taarifa kwa kina zinaendelea kutoka mamlaka husika....

Kamishna Msaidizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete amesema kuwa, moto uliozuka na kuanza kuteketeza sehemu ya hifadhi za Mlima Kilimanjaro, huenda wakafanikiwa kuuzima leo baada ya hapo jana kushindikana na kuendelea kuwaka usiku kucha.

Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 12, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio na kusema kuwa zoezi la kuuzima moto huo litakapokamilika shirika hilo litatoa tathmini ya hasara iliyojitokeza.

"Kama TANAPA tumefanya juhudi kubwa sana na asubuhi ya leo vikosi mbalimbali vimefika Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya zoezi hilo la kuuzima moto, na kazi ya kuuzima moto huo inaendelea na tunatarajia kwa nguvu hiyo iliyopelekwa moto huo utaweza kudhibitiwa kuzima kwa siku ya leo,"amesema Shelutete.

"Bado tunaendelea kufanya tathmini na baadaye tutatoa taarifa kamili juu ya chanzo na madhara ambayo yamejitokeza, kipaumbele kwanza tunashughulikia masuala ya uzimaji wa moto halafu mengine yatafuata baadaye,"amesema.

Moto huo ambao hadi sasa unaendelea kuteketeza sehemu ya Mlima Kilimanjaro ulizuka jana mchana ya Oktoba 11 mwaka huu na mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, endelea kufuatilia Diramakini kwa mrejesho zaidi.

 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news