Msajili wa Vyama vya Siasa nchini asema mpango wa Oktoba 3 ni batili, awaonya waliokusudia kuungana

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza amevitaka vyama vya siasa vinavyotaka kuungana Oktoba 3, mwaka huu kuacha mara moja mpango huo,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza.

Amesema, mpango huo unakiuka utaratibu wa sheria na kwamba walianza vizuri hivyo ni vyema kila mmoja akaendelea kunadi sera zake kuelekea Oktoba 28,mwaka huu.

"Kwanza tunaawaasa hao wanaotaka kufanya hivyo tarehe 3, sisi kama walezi wa vyama vya siasa kwa sababu wanakiuka sheria, walianza vizuri hivyo kila mmoja aendelee kunadi sera yake na wagombea wao wa urais,"ameema Nyahoza.

Nyahoza ametoa rai hiyo leo Oktoba Mosi, 2020 kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio.Amesema kuwa,tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekwishaviandikia barua vyama hivyo kwa kuwa ni masuala ya kiofisi hivyo huwa hawaziweki barua hizo hadharani.

Amesema, sheria ya vyama vya siasa inawekwa kwa maslahi ya wanachama na wananchi na unapotaka kushirikiana hutakiwi kufanya kitendo chochote kinachohadaa wananchi kwa hiyo ni kosa kufanya hivyo ghafla wakati wa uchaguzi.

“Ukiunganisha nguvu na chama kingine wakati mmeshakubaliana na wananchi kwamba mtatekeleza sera gani ni kuwahadaa, sisi tulishawasiliana nao na tukawaambia waache,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news