Mtibwa Sugar SC, Coastal Union zapeta michuano ya leo

Mtibwa Sugar SC leo Oktoba 19,2020 imeichapa Namungo FC 1-0, kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa CCM mjini Gairo, Morogoro, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kiungo Salum Kihimbwa kwa penalti 76' ndiye aliyewezesha bao hilo la mwanzo na mwinsho ambalo liliwezesha Mtibwa Sugar SC kuibuka na alama tatu.

Chini ya kocha wa muda, Vincent Barnabas ambaye ni mchezaji wa zamani wa Mtibwa kama Zuberry Katwila aliyekuwa anainoa timu hiyo na kuachana nao ndani ya siku moja, Mtibwa Sugar wanafikisha alama nane baada ya kucheza mechi saba, hivyo kutoka nafasi ya 15 hadi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu huku Namungo FC ikibaki nafasi ya nane kwa alama tisa.

Wakati huo huo, Coastal Union imeichapa Biashara United 3-0, mabao ya Hamad Rajab 32' na Raizin Hafidh 45' na 61' ndani ya Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ndiyo yaliyowezesha matokeo hayo.

Katika mechi nyingine, Jabir Aziz 85' kupitia penalti ameinusuru JKT Tanzania kulala mbele ya Polisi Tanzania iliyotangulia kwa bao la Jumanne Elfadhili 21' baada ya timu hizo kutoa sare ya 1-1 Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news