Shule za msingi na sekondari 83 kutoka kata 15 katika wilaya tatu za Nyang'hwale,Chato na Geita mkoani Geita zimenufaika na matenki ya kutunzia maji shuleni kutoka shirika lisilo la kiserikali la Plan International,anaripoti Robert Kalokola,(Diramakini) Geita.
Meneja wa Miradi wa Shirika la Plan International Mkoa wa Geita, Adolf Kaindoa amesema kuwa shirika hilo limekabidhi matenki 83 yenye ujazo wa lita 1,000 kila moja huku yakiwa na mifuko 166 ya saruji ambapo jumla yana thamani ya shilingi milioni 24,153,830.
Amesema, lengo la kutoa matenki hayo ya kukinga maji ni kupunguza utoro shuleni hasa kwa wanafunzi wa kike wanapokuwa kwenye hedhi.Ameongeza, sababu nyingine ni kupambana na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu,homa ya matumbo na kuhara damu.
Meneja Kaindoa amesema kuwa, utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mtakwimu Mkuu wa Serikali na Shirika la UNICEF zilionyesha upungufu wa maji shuleni katika Mkoa wa Geita ni asilimia 47.7 , Kagera asilimia 55.2, Mwanza asilimia 54.6 na Kigoma asilimia 49.9.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema, matenki hayo yametolewa ikiwa ni matokeo ya shirika hilo kufanya utafiti na kugundua tatizo.
Amepongeza Plan International kwa kutoa msaada kutokana na utafiti huku akiomba wadau wengine kuiga utaratibu huo wa Shirika la Plan International la kufanya kazi kwa kuanza na utafiti.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Wilson Shimo amesema kuwa, upatikanaji wa maji shuleni katika wilaya hiyo ni asilimia 45. Amesema, msaada huo wa matenki ya kutunzia maji utasaidia kupunguza tatizo hilo katika wilaya hiyo kwa shule za msingi na sekondari.
Shirika la Plan International linatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Shirika la SEDIT, Shirika la Kivulini pamoja na Serikali ya Mkoa wa Geita kuanzia mwaka 2012 hadi 2023 katika Mkoa wa Geita.
Shule inapatiwa tenki moja la kutunzia maji pamoja na mifuko miwili ya saruji kwa ajili ya kujengea stendi za kuwekea tenki.Mradi huo pia umewapa mafunzo walimu wapatao 330 kutoka shule 83 katika mradi wa ulinzi na usalama wa mtoto na usafi mazingira shuleni.
Mradi huo unaotekelezwa kwa ajili kusaidia kutokomeza ajira hatarishi kwa mtoto,ulinzi na usalama wa mtoto na usafi wa mazingira umeshatumia shilingi 49,306,830.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akifurahia na mwanafunzi baada ya kupokea matenki ya kutunzia maji kutoka Plan International.Wengine ni Meneja wa Miradi Adolf Kaindoa (nyuma ya mwanafunzi) na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Wilson Shimo (kushoto). (DIRAMAKINI).Shirika hilo limetoa matenki hayo kwa shule za msingi na sekondari kwa wilaya ya Nyang'hwale (kata 4),Chato (kata 7) na Geita (kata 4) katika vijiji 63.
Meneja wa Miradi wa Shirika la Plan International Mkoa wa Geita, Adolf Kaindoa amesema kuwa shirika hilo limekabidhi matenki 83 yenye ujazo wa lita 1,000 kila moja huku yakiwa na mifuko 166 ya saruji ambapo jumla yana thamani ya shilingi milioni 24,153,830.
Amesema, lengo la kutoa matenki hayo ya kukinga maji ni kupunguza utoro shuleni hasa kwa wanafunzi wa kike wanapokuwa kwenye hedhi.Ameongeza, sababu nyingine ni kupambana na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu,homa ya matumbo na kuhara damu.
Meneja Kaindoa amesema kuwa, utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mtakwimu Mkuu wa Serikali na Shirika la UNICEF zilionyesha upungufu wa maji shuleni katika Mkoa wa Geita ni asilimia 47.7 , Kagera asilimia 55.2, Mwanza asilimia 54.6 na Kigoma asilimia 49.9.
Meneja wa Miradi wa Shirika la Plan International Mkoa wa Geita, Adolf Kaindoa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (hayupo pichani) kuhusu msaada wa matenki 83 na mifuko 166 ya saruji. (DIRAMAKINI).Ameongeza kuwa, wanafunzi wa kike wanashindwa kwenda shule katika siku ambazo ndani ya mwezi anakuwa kwenye hedhi baada ya kukosa maji shuleni kwa ajili ya kujistiri. Amesema kuwa,matenki hayo yatasaidia kupata maji kwa ajili ya kunywa,kufanya usafi,pamoja na kusaidia shule ambazo zina mpango wa chakula shuleni kupata maji ya uhakika.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema, matenki hayo yametolewa ikiwa ni matokeo ya shirika hilo kufanya utafiti na kugundua tatizo.
Amepongeza Plan International kwa kutoa msaada kutokana na utafiti huku akiomba wadau wengine kuiga utaratibu huo wa Shirika la Plan International la kufanya kazi kwa kuanza na utafiti.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akinyanyua mfuko wa saruji kumkabidhi Afisa Elimu Wilaya ya Geita katika tukio la Shirika la Plan International kukabidhi matenki 83 na mifuko 166 ya saruji kwa shule za sekondari na msingi 83 Mkoa wa Geita. (DIRAMAKINI).Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameomba shirika hilo kuendeleza juhudi za mradi huo ili kuhakikisha shule nyingi zaidi zinafikiwa na maji.

Tags
Habari