Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amezindua kitabu cha “Mwalimu bora wa Soka’ na kusema kuwa kitabu hicho ni chuo kwa wachezaji wa mpira wa miguu pamoja na walimu wa mchezo huo ndani na nje ya Zanzibar.
Rais Dkt.Shein ameyasema hayo leo Oktoba 9,2020 huko katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil, Kikwajuni jjini Zanzibar katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho kilichoandikwa na Kocha Gullam Abdalla Rashid, hafla ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na Serikali pamoja na wanamichezo wakiwemo wanasoka wakongwe wa Zanzibar.
Katika maelezo yake Rais Dkt.Shein ambaye pia, aliwahi kuwa mwanamichezo maarufu hapa Zanzibar katika ujana wake amesema kuwa, kitabu huandikwa ili kisomwe, hivyo anaamini kuwa kitabu hicho kitavutia idadi kubwa ya wasomaji kwa sababu mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini una mashabiki wengi.
Amesema kuwa mwandishi wa kitabu hicho hakukiandika kwa kubahatisha bali amekiandika kwa umahiri na weledi mkubwa kwa sababu yeye ni mwanasoka wa zamani sana tangu anasoma skuli ya msingi ya Gulioni hapa Zanzibar.
Amesema kuwa mtunzi wa kitabu hicho Kocha Gullam Abdalla Rashid amecheza mpira katika vilabu maarufu hadi timu ya Taifa ya Zanzibar na Taifa ya Tanzania ambapo mafanikio hayo ameyapata kutokana na heshima na nidhamu kubwa katika soka.
“Ni mtu mwenye nidhamu sana, na hakuwahi kumpiga mtu kibuyu hata siku moja wakati akicheza mpira kwani alikuwa anacheza mpira kwa ustaarabu mkubwa,”amesema Dk. Shein.
Aidha, Rais Dk. Shein amempongeza na kumshukuru Kocha Gullam kwa kumchagua yeye kuwa mwandishi wa dibaji ya kitabu chake hicho ambapo Dk. Shein alieleza kuwa kitabu hicho kitatoa mchango mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla kwa kuwahamasisha wapenzi wa mpira wa miguu ili wawe walimu bora.
Ameongeza kuwa fani ya michezo inahusisha mafunzo ya vitendo pamoja na taaluma ya nadharia na vitendo na nadharia vikiunganishwa pamoja vinaleta ufahamu unaokamilika, hivyo kitabu hicho kitampelekea msomaji anayekisoma na baadae akaingia kiwanjani kujua nini anachokifanya katika mpira wa miguu.
Hivyo, Rais Dk. Shein ametoa wito kwa wanamichezo wote kukinunua kitabu hicho hasa ikizingatiwa kwamba kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kwani hilo linafaida yake kwa mwanasoka au mshabiki wa soka wa hapa hapa nchini iwapo anajua kusoma na kwa vile anaamini wengi wao wanajua kusoma hivyo watafaidika wka kiasi kikubwa.
Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein amesema kuwa tayari Kocha Gullam ameshafungua milango kwa wenziwe wengine waweze kuandika zaidi na kusisitiza haja kwa wengine kuandika historia ya mchezo wa mpira wa miguu hapa Zanzibar, kuandika kuhusu wapenzi, mashabiki na mpezi bora wa mpira wa miguu.
Ameeleza kuwa maarifa na ujuzi mkubwa katika michezo ni jambo muhimu sana kwa mchezaji kuwa nayo lakini hata hivyo ili kuyapata maarifa na ujuzi kunahitajika kuwepo miundombinu bora vikiwemo viwanja vya kujifunzia na kufanyia mazoezi na ndio maana Serikali anayoiongoza ikafanya juhudi ya kuhakikisha hilo linaimarika.
Katika maeelezo yake Rais Dkt. Shein pia, alisisitiza haja ya kuwaandaa vijana katika soka kwani nchi mbali mbali duniani zilizopata mafanikio zimeanza na utaratibu huo hivyo, ipo haja ya kuwaandaa vijana na ndio maana Serikali imeshaanzisha mchakato.
Amesisitiza kwamba suala la kuhifadhi miundombinu ya michezo ni jambo lililoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo, ni jambo la faraja kuona kwamba juhudi za kuhusisha tasnia ya michezo Zanzibar zimeleta mafanikio.
Dkt. Shein pia ametumia fursa hiyo kukitaka Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), kubadilika hasa katika uongozi wake ili michezo iweze kufanikiwa hapa nchini.
Rais Dk. Shein alimsisitiza Kocha Gulam kuendelea kutunga vitabu vyengine na yeyote yule ambaye yuko tayari kutunga yeye atashirikiana nae kwani na yeye kwa upande wake ameshaanza kuandika mambo kadhaa kuhusu michezo hapa nchini.
Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwepo uzalendo wa kuzibeza timu za nyumbani badala ya kuzifuatilia zaidi timu za Ulaya huku akieleza haja ya timu kuziita majina ya nyumbani.
Nae Waziri Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ali Abeid Karume alsiema kuwa kitabu hicho kitakuwa nguzo muhimu kwa wale wote watakao taka kujifunza soka.
Ameongeza kuwa kitabu hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya mpira wa miguu hapa Zanzibar na kuweza kusaidia kusimamia soka.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Omar Hassan King kwa upande wake ametoa pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa kufanikiwa kuimarisha sekta ya michezo katika uongozi wake ndani ya miaka kumi.
Ameeleza kuwa ndani ya miaka kumi ya uongozi wa Dk. Shein amefanya mambo mengi katika kuimarisha michezo ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya michezo hapa nchini kwa kuvijenga upya viwanja vya michezo na vyengine kuvifanyia ukarabati mkubwa kama vile kiwanja cha Mao tze Dong, Gombani na kwianja cha Amani.
Pia, ameanzisha viwanja katika Wilaya za Zanzibar ambavyo vipo baadhi tayari vimeshaanza kutumika kama vile kiwanja cha Kitogani Wilaya ya Kusini Unguja, kiwanja cha Kishindeni Wilaya ya Micheweni na Kangani Wilaya ya Mkoani.
Amesema kuwa Zanzibar imeimarika kutokana na kuongezeka kwa michezo, kufufua FA Cup na kufufua vuguvugu michezo maskulini na kuanzisha Idara za micehzo na kuongeza wataalamu wa michezo huku akieleza kuwa kuwepo wka siku maalum ya mazoezi ya tarehe mosi Januari ya kila mwaka pia ni ubunifu wake Rais Dk. Shein.
Mapema akisoma Wasifu wa Mwandishi na Maelezo ya Kitabu hicho Mwalimu Suleiman Mamoud Jabir alisema kuwa Kocha Gulam ni mwanamichezo wa muda mrefu ambaye aliwahi kuwa mchezaji, mwalimu na hatimae kuwa kiongozi katika taasisi mbali mbali za michezo ndani na nje ya Zanzibar.
Amesema kuwa kitabu hicho alichokitunga kina Sura 11 ambazo kila Sura imeeleza mambo mbali mbali kuhusu mpira wa miguu, ukocha ama utaalamu, ufundishaji, mpango wa mazoezi na mafunzo katika msimu wa mchezo huo, umuhimu wa uzima wa mwili, ustadi na umakini katika soka pamoja na mambo mengineyo ya soka.
Nae Mtunzi wa Kitabu hicho Kocha Gulam Abdalla Rashid alitoa pongezi na shukurani wka Rais Dk. Shein kwa kumuunga mkono katika utungaji wa kitabu chake hicho pamoja na kuwashukuru watu mbali mbali waliomsadia akiwemo mwanawe na familia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) akinyanyua kitabu cha "Mwalimu Bora wa Soka" baada ya kukizindua rasmi leo Oktoba 9,2020 katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar ambacho kimeandikwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Kocha Gulam Abdalla. (IKULU/Diramakini).