RC GEITA: MAUZO YA DHAHABU WACHIMBAJI WADOGO GEITA YAMEVUNJA REKODI

Mkoa wa Geita umevunja rekodi kwa kukusanya kilo 497 kwa mwezi wa tisa kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo zenye thamani ya shilingi Bilioni 62.96 zilizouzwa katika masoko tisa mkoa mzima katika wilaya zote za Geita,Chato, Nyang'hwale,Bukombe na Mbogwe,anaripoti Robert Kalokola (Diramakini),Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akitoa takwimu za ongezeko la mauzo ya Dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo katika Mkoa wa Geita kwa mwezi Septemba,mwaka huu hadi kufikia Bilioni 62.96 (Diramakini).


Ongezeko hilo la mauzo makubwa ya Dhahabu limewezesha Serikali imekusanya mapato yake jumla ya Bilioni 4.88 na Halmashauri zimekusanya tozo za huduma milioni 188 kwa mwezi mmoja.

Soko la Dhahabu la Kalangalala peke yake ambalo liko Halmashauri ya Mji wa Geita limefanikiwa kufikia kiwango cha kufanya Biashara ya Bilioni 2 kwa siku moja ya kuuza Dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel leo Oktoba 8,2020 ofisini wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari wakati akitoa mwelekeo wa mafanikio ya sekta ya madini katika mkoa huo.

Amesema, mafanikio hayo yamechagizwa kwa kiwango kikubwa na juhudi za wabunge wa Mkoa wa Geita,mabaraza ya madiwani,watendani wa wizara ya madini na tume ya madini na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutekeleza maelekezo ya Rais John Magufuli.

Robert Gabriel amesema kuwa, mapato yanayo tokana na biashara ya mauzo ya Dhahabu yamewezesha Halmashauri kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwenye sekta ya Afya , elimu,Masoko ,miundombinu ya barabara na huduma nyingine za kijamii.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amefafanua kuwa,sekta ya madini italeta mageuzi makubwa kiuchumi katika mkoa huo pamoja na taifa kwa ujumla kwasababu mapato yake yanachangia kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini katika Soko la Dhahabu Geita mjini, Situmaini Ngalama amesema kuwa, ongezeko hilo la mauzo makubwa ya Dhahabu yanatoka navudhibiti mkubwa wa serikali .

Amefafanua kuwa,baada ya serikali kuanzisha masoka ya kuuza na kununulia madini imeongeza udhibiti wa utoroshaji wa madini hivyo mauzo yote kufanyika katika soko halali.

Amesema, kwa sasa utoroshaji wa madini haupo kwa sababu vyombo vingi vya ulinzi vimedhibiti maeneo yote kwahiyo wafanyabiashara wameachana na tabia hiyo hasa kwa kuhofia kufilisiwa na kufungwa.

Amesema, changamoto zilizokuwepo nyingi serikali imezitatua na zilizopo kwasasa ni zile ambazo ziko kwenye nchi ambazo ndiyo soko lao kuendelea kukabiliwa na covid-19 hadi Sasa hivyo kuwa na masharti ya kuingia.

Mfanyabiashara Adili Said anasema, kwa sasa makusanyo yameongezeka na Dhahabu inapatikana kwa wingi lakini bado wafanyabiashara bado wanaomba uzalishaji uongezeke maana wanunuzi wamekuwa wengi katika soko kulinganisha na wanaokuja kuuza.

Mkoa wa Geita unatajwa kuwa kinara nchini kwa kuzalisha Dhahabu nyingi huku sekta ya wachimbaji wadogowadogo ikiendelea kuonyesha kukua kwa kasi kubwa na kuchangia mapato ya serikali hasa baada ya mabadiliko ya sheria ya madini yaliyofanyika mwaka 2017 na uanzishwaji wa masoko ya madini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news