Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema kuwa, zoezi la kuzima moto uliolipuka ghafla mchana wa Jumapili ya Oktoba 11, 2020 kwenye Mlima Kilimanjaro linaendelea, anaripoti Mwandishi Diramakini.
"Ili kuongeza ufanisi wa zoezi hilo, leo mchana tumeanza kutumia helikopta. Juhudi zinaendelea kufanywa na Serikali kwa kushirikiana kwa karibu na wadau wengine ili kuongeza ndege kusaidia zoezi hilo,"Waziri Kigwangalla ameeleza hayo leo Oktoba 15, 2020.
Amesema kuwa, "tunapenda kuwajulisha wadau wa utalii na wageni wanaotaka kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kuwa, shughuli za kupanda mlima zinaendelea kufanyika kama kawaida.
"Kwa niaba ya Serikali, napenda kutoa shukurani za dhati kwa wadau mbalimbali wanaoshirikiana nasi katika kusaidia zoezi la kuzima moto huu.Tutaendelea kutoa taarifa kwa umma katika kila hatua,"ameongeza Waziri huyo.
Serikali yaongeza kasi kudhibiti moto Mlima Kilimanjaro
Tags
Habari