Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa, Serikali mpya ya Sudan imekubali kuilipa Marekani dola milioni 335 kwa ajili ya waathirika na familia zilizoguswa na vitendo vya kigaidi,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ameyasema hayo leo Oktoba 19,2020 kupitia taarifa iliyoonwa na Mwandishi Diramakini katika ukuta wake wa Facebook.
"Habari njema,Serikali mpya ya Sudan iliyopo katika mchakato imekubali kulipa dola milioni 335 kwa Marekani kwa ajili ya waathirika na familia zilizoguswa na ugaidi.
"Pindi watakapofanya malipo hayo, nitaiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa magaidi, hii ni hatua kubwa kwa ajili ya haki ya Wamarekani na hatua muhimu kwa Sudan,"ameeleza.