"Tunamtaka Bwana na Nguvu zake. Taarifa za awali za mazishi ya Mzee wetu wa Imani Rev. Wilson Kimaro ni kama ifuatavyo:
1. Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 7 Oktoba 2020 huko Arusha.
2. Familia inaendelea kufuatilia kibali ili iliwezekana Mpendwa wetu azikwe kwenye eneo la makazi/nyumbani kwake Ngaramtoni.
3. Shughuli zote za Ibada ya Mazishi (kuaga, rambirambi nk) zitafanyikia TAG Calvary Temple - Arusha ili kuruhusu tu watu wachache kwenda eneo la mazishi kwa sababu ya ufinyu wa eneo hilo.
4. Ratiba kamili ya Shughuli nzima ya siku hiyo ya Jumatano itafuata hapo baadae.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe.
Rev. Dr. Boniface Mgonja
KATIBU MKUU
Tags
Habari