Tetesi: Manchester United, Manchester City, Liverpool zatambiana,

Kwa mujibu wa Tuttomercato, Maurizio Sarri ambaye alikuwa mkufunzi wa Juventus na Chelsea ni mgombea wa nafasi ya meneja wa Klabu ya Fiorentina. 

Huku AS ikiripoti kuwa,aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Memphis Depay (26) anasema kwamba, baadhi ya sheria zilimzuia kujiunga na Barcelona katika dirisha la uhamisho.

Sky sports inaripoti kuwa,kiungo wa Ufaransa,Michael Cuisance (21) amefutilia mbali madai kwamba kufeli kwa vipimo vya matibabu ndio sababu iliyosababisha kushindwa kwa uhamisho wake kujiunga na Leeds, kiungo huyo baadaye alijiunga na Marseille kwa mkopo kutoka Bayern Munich. 

Nayo Liverpool itafanya mazungumzo na winga Harry Wilson kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mkopo katika klabu nyingine hii ikiwa ni kwa mujibu wa Standard.

Football Insider inaripoti kuwa, klabu ya
Bournemouth haitamruhusu kiungo wa kati David Brooks (23) kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho. Sheffield United inamtaka mchezaji huyo.

Klabu ya West Ham inafikiria usajili wa £5m wa kiungo wa kati wa QPR na Ireland Ryan Manning (24). Kwa mujibu wa Star mchezaji huyo pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto katika klabu hiyo.

Guardian inaripoti kuwa,The Hammers wanataka kumsaini mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Josh King (28), lakini wanaamini The Cherries inafaa kupunguza dau wanaloitisha la £17milioni.

Sky sports inaripoti kuwa,mshambuliaji wa Wales Gareth Bale (31) anataka kushinda taji la Uingereza msimu huu akiichezea Tottenham.

Kwa upande wa Mail,Klabu ya Arsenal inataka kuanzisha mazungumzo na Mesut Ozil kuhusu kufutilia mbali kandarasi yake kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari, mwakani.

Times inaripoti kuwa,Manchester City imepiga hatua katika mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bryune.Wanataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutia saini kandarasi nyingine ya miaka minne.

Pia Sun inaripoti kuwa,Manchester United itajaribu kumsaini beki wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 21, kwa dau la £36.5m msimu ujao. Liverpool na Manchester City zina shauku ya kumsajili.
Dayot Upamecano

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news